Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda akitoa maelekezo kwa wajumbe wa kamati ya Siasa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo wakati wakikagua moja ya caravati linalojengwa katika Barabara ya Maluga Mtaa Saba -Misuna na Mgungia hadi Kaselya wakati kamati hizo zilipokuwa zikikagua miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake Tarafa ya Shelui wilayani humo jana.
Mkzi wa Kijiji cha Maluga akiishukuru Serikali na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa shule hiyo. |
Na Dotto Mwaibale, Singida.
Mwenda ametoa agizo hilo jana wakati akiwahutubia Wananchi wa Tarafa ya Shelui kwenye mkutano wa hadhara baada ya kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo kumaliza kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Tarafa hiyo.
"Serikali haiwezi kuvumilia kuona wanafunzi waliofaulu kwenda kuanza Sekondari hawaendi shuleni licha ya kutumia fedha nyingi ya kuboresha mazingira bora ya kupata elimu hivyo naagiza kuanzia leo Machi 30, 2022 hadi ifikapo Aprili 30, 2022 watoto hao wawe wamepelekwa kuanza masomo na wazazi watakao kahidi agizo hilo tutawachukulia hatua kali" alisema Mwenda.
Akizungumzia ukaguzi wa miradi hiyo iliyogharimu zaidi ya Sh.9 Bilioni alisema kamati hizo zilifanya ukaguzi huo ili kuona nini kimefanyika katika mwaka mmoja wa uongozi wake Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi katika Tarafa hiyo ambapo waliridhishwa na utekelezwaji wake.
Alisema baada ya kuiona walipanga kufanya mkutano huo wa hadhara ili kuwaeleza wananchi mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu kuwa madarakani.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara hiyo Mwenda alisema miradi hiyo inafanyika ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali inawajibu wa kuikagua ili kuona kama inatekelezwa kwa viwango vinavyo kubalika.
Alisema Serikali inatumia fedha nyingi kuitekeleza akitolea mfano ujenzi wa madarasa yaliyotokana kwa fedha za mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19 ambayo yamewaondolea adha kubwa ya michango wananchi ya kuchangia ujenzi na ununuaji wa madawati.
Mwenda alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo na kuwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kuitunza.
Aidha Mwenda aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa vijana wanaoshiriki katika zoezi la anuani za makazi na postikodi linaloendelea nchi nzima kwa kuwaelekeza majina ya mitaa na mambo mengine yanayohitajika na akawaomba kufanya hivyo pia katika zoezi la Sensa ya watu na makazi.
Mwenda aliwapongeza wananchi wa Tarafa hiyo kwa kuitikia katika kilimo ambapo mazao mengi yanaonekana kustawi ambapo aliwataka kujiadhari na walanguzi ambao wameanza kupita kwa wakulima kuwashawishi ili wanunue mazao yao yangali shambani kwa bei ya ulanguzi.
Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Samuel Ashery aliwaomba wananchi ilipo miradi hiyo kuitunza na akawataka wakandarasi kuikamilisha kulingana na thamani ya fedha walizopewa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi aliwaomba wakandarasi waliopewa kuijenga miradi hiyo kuijenga kwa wakati kama walivyo kubaliana kwenye mikataba ili wananchi waweze kuanza kuitumia kwa wakati.
Baadhi ya miradi iliyokaguliwa na kamati hizo ni ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Maluga kwa gharama ya Sh.470 Milioni, ujenzi wa bweni moja kwa ufadhili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tumaini aambao uligharimu Sh.75 Milioni, ukamilishaji wa Jengo la Zahanati ya Ulemo ambapo walipokea Sh.50 Milioni na ujenzi wa mradi wa wa vyoo na uwekaji wa miundombinu ya ya maji ndani ya Zahanati ya Misigiri kwa gharama ya Sh. 25.2 Milioni.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni ujenzi wa barabara za Maluga-Mtaa wa Saba, Mtaa saba- Misuna na Mgungia-Kaselya kwa gharama ya Sh.492,019,500 fedha zilizotoka Serikali Kuu, ujenzi wa mradi wa nyumba za Watumishi katika Zahanati ya Shelui kwa gharama ya Sh.90,000,000 ambao unahusisha jengo moja lenye nyumba tatu za watumishi, ujenzi wa Kituo cha Afya Mtoa ambacho kitagharimu Sh.400,000,000 na ukamilishaji wa vyumba viwili vya maabara Shule ya Sekondari Mtoa.
Mwenda alitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa mradi wa maji Kijiji cha Wembereambao umetengewa bajeti ya Sh. 356,080,529 na matengenezo ya barabara ya Shelui kwenda Tintigulu.
No comments:
Post a Comment