TANROADS Lindi Waendelea Kurejesha Mawasiliano Ya Barabara Ya Lindi – Dar- es Salaam - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, May 5, 2024

TANROADS Lindi Waendelea Kurejesha Mawasiliano Ya Barabara Ya Lindi – Dar- es Salaam

Timu ya Watalaamu wa Wakala ya Barabara (TANROADS) na Wakandarasi wanaendelea na kazi ya kurejesha miundombinu ya Barabara ya Lindi – Dar- es Salaam ambayo imeharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zikiambatana na kimbunga Hidaya.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Lindi Mha. Emil Zengo ameyasema hayo leo tarehe 5 Mei 2024 alipotembelea na kukagua uharibifu uliotokea katika eneo la Somanga – Mtama.
Amesema kuwa leo majira ya asubuhi maji yamefurika kwa wingi na kuharibu eneo la takribani mita 80 katika barabara ya Somanga – Mtama na kukata tuta la barabara hiyo eneo la Mikereng’ende umbali wa Kilomita 10 kutokea Somanga uelekeo wa Lindi.

Pia imeleta athari katika eneo la Lingaula umbali wa kilomita 12 kutokea Nangurukulu uelekeo wa Lindi

Amesema kuwa jitihada za Serikali zinaendelea kufanywa ili kurejesha mawasiliano ya barabara hiyo kutokea upande wa Mkoa Pwani na kutokea Lindi.

Mhe. Zengo ametoa wito kwa Wananchi na Madereva kuendelea kuwa na subira kwani Serikali kupitia TANROADS inaendelea kufanya kila linalowezekana kurejesha miundombinu ya barabara hiyo na kuwezesha Wananchi kupata huduma ya usafiri katika barabara kama kawaida.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages