BRELA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUJISAJILI ILI KUCHANGAMKIA FURSA KIBIASHARA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, June 5, 2024

BRELA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUJISAJILI ILI KUCHANGAMKIA FURSA KIBIASHARA

Afisa Sheria za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (Brela) Lupakisyo Mwambiga wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii yanayofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga.
Na Oscar Assenga, TANGA

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELA) umewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kujisajili na wakala huo kutokana na kwamba kama haujasajiliwa hauwezi kuomba tenda rasmi ambazo zinatangazwa na Taasisi mbalimbali za Serikali na Idara zake.

Hayo yalisemwa leo na Afisa Sheria za Wakala huo Lupakisyo Mwambiga wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 11 ya Biashara na Utalii yanayofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga.

Lupakisyo alisema kwamba ni vema wafanyabiashara na wajasiriamali kuona umuhimu wa kurasimisha biashara zao kwa kusajili brela na kupata leseni inayostahili ili waweze kutekeleza majukumu yao.

Wengi wanachanganya leseni kati ya daraja A na B ambazo zinatolewa na halmashauri na Manipsaa kuna biashara zenye sura ya kitaifa na kimataifa unatakiwa kupata leseni kutoka brela hivyo nawahimiza wafanyabishara waje kupata elimu kwa kueleza biashara wanazofanya" Alisema.

Kwa lengo la kushauriwa ni leseni gani anapaswa kuomba kutoka brela na wale wafanyabiashara wenye viwanda vidogo vidogo tunatoa leseni za viwanda watu wengi hawajua unapoanzisha viwanda lazima uwe na leseni kutoka Brela” Alisema.

Alisema kwamba kuna leseni ya uanzishwaji wa kiwanda na leseni biashara kwa wajasirimali wenye viwanda vidogo na wafanyabiashara wenye viwanda vikubwa huku akiwataka kutembelea banda lao ili waone ni vitu gani wanaweza kufanya kupata leseni.

Hata hivyo alisema kwamba wapo kushiriki kwenye maonyesho ya biashara na utalii kutokana na kwamba ni moja ya taasisi za kusimamia usajili wa biashara pamoja na leseni na wamekuja kutoa elimu na huduma za papo kwa papo ikiwemo usajili wa kampuni, majina ya biashara.

Alisema pia wanatumia maonyesho hayo kutoa leseni kundi A na utoaji wa leseni za viwanda na usajili wa alama za biashara kwa wateja wao huku akiwataka wananchi wa mkoa wa Tanga kuendelea kujitokeza kufika kwenye banda lao ili wawez kupata ushauri jinsi gani wanaweza kusajili kampuni ,jina la biashara au alama ya bisharaa na waliokuwa tayari wanasajiliwa kupitia mtandao kwa kuwasaidia kwa sababu wapo kwenye maonyesho na wamekuwa wakitoa elimu kwa wafanyabiashara umuhimu wa kusajili au kurasimisha biashara maana wengi mpaka wakipata changamoto Fulani ndio wanakilimbia brela.

Wengi mpaka wanapopata changamoto ndio wanakimbili brela labda amepata tenda unatakiwa kupeleka cheti kutoka brela ndio wanahangaika kusajili au benki wakitaka taarifa kuhusu brela ndio wanakwenda kusajili” Alisema.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages