INEC YAWANOA WASIMAMIZI WA VITUO VYA UCHAGUZI JIMBO LA KWAHANI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, June 4, 2024

INEC YAWANOA WASIMAMIZI WA VITUO VYA UCHAGUZI JIMBO LA KWAHANI

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Dkt.Zakia Mohamed Abubakar leo tarehe 04 Aprili, 2024 wakati akifungua mafunzo kwa Makarani waongozaji Wapiga Kura vituoni yanayofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba, Mjini Magharibi-Unguja Zanzibar.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Dkt.Zakia Mohamed Abubakar leo tarehe 04 Aprili, 2024 wakati akifungua mafunzo kwa Makarani waongozaji Wapiga Kura vituoni yanayofanyika katika Skuli ya Sekondari ya Lumumba, Mjini Magharibi-Unguja Zanzibar.
Washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku mbili.
Washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku mbili.
Wasimamizi na wasimamizi wasaidizi ngazi ya vituo wakila kiapo chankujitoa uanachama wa Chama cha siasa na kile cha kutunza siri kabla ya kuanza mafunzo yao.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar

Wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya Kupiga Kura Jimbo la Kwahani Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar wametakiwa kufanya kazi kwa kujiamini, uadilifu na weledi wanapotekeleza majukumu yao ya uchaguzi kutokana na dhamana waliyopewa na Tume.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Dkt.Zakia Mohamed Abubakar wakati akifungua mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya vituo yanayofanyika kuanzia leo tarehe 5 hadi 6 Juni, 2024 Skuli ya Sekondari ya Lumumba, Mjini Magharibi- Zanzibar.

Mnatakiwa kutambua kuwa mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu ya Imani ya Tume kuwa mnao uwezo wa kufanya kazi hii, Jambo muhimu mnalotakiwa kulizingatia ni kujiamini na kufanya kazi kwa weledi, na kwamba katika utendaji wa majukumu yenu mnapaswa kuzingatia Katiba ya Nchi, Sheria za Uchaguzi na Kanuni zake, Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume,” alisema Mh. Dkt. Zakia.

Mhe. Dkt Zakia amesema, kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume imepewa jukumu la kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hii ni pamoja na Chaguzi ndogo zinazojitokeza kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo vifo kama ilivyotokea katika Jimbo la Kwahani.

Hata hivyo, pamoja na kuwa Tume ndiyo yenye jukumu hilo, wanaoratibu na kusimamia Uchaguzi ngazi ya Vituo ni nyinyi tuliowateua pamoja na watendaji wengine”.

Aidha, Mhe. Dkt Zakia amesema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kufuatwa na kuzingatiwa kwani hatua na taratibu hizo ndio msingi wa Uchaguzi kuwa mzuri, wenye ufanisi na hivyo kupunguza kama siyo kuondosha kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa Uchaguzi.

Amewataka washiriki hao wa mafunzo kuwa watulivu na kupokea mada zitakazowasilishwa, wabadilishane uzoefu na kujadili namna ya kufanikisha Uchaguzi katika Jimbo la Kwahani.

Nachukua fursa hii kuwaasa kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katikauendeshaji wa Uchaguzi, mhakikishe mnazingatia maelekezo mtakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea,” alisema Mhe.Dkt Zakia.

Aidha, amewataka kuhakiki vifaa watakavyovipokea kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi na kuhakikisha kila Msimamizi wa Kituo anapata vifaa vyote vya Uchaguzi vinavyohitajika mapema.

Pia, Mhe. Dkt. Zakia amewasisitiza kuwa siku ya Uchaguzi mnaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha Kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufanya mawasiliano na Msimamizi wa Uchaguzi pale ambapo utahitajika ushauri kuhusiana na masuala ya Uchaguzi uliopo.

Kabla ya kufungua Mafunzo hayo, wasimamizi hao na wasimamizi wasaidizi hao walikula kiapo cha kutunza Siri na Kujitoa uachama wa Chama cha Siasa mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kwahani Bi.Safia Iddi Muhammad.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza siku ya Jumamosi ya tarehe o8 Juni, 2024 kuwa ni siku ya uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kwahani. Vyama 14 vya siasa vimejitokeza na vinaendelea na kampeni kuelekea siku ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages