JE UNALIFAHAMU GARI AINA YA AJBAN 440A? - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, March 30, 2017

JE UNALIFAHAMU GARI AINA YA AJBAN 440A?



AJBAN 440A ni aina ya gari la Kivita maalum kabisa lililobuniwa na kutengenezwa na kampuni ya magari ya Kivita iitwayo NIMR Automotives, iliyopo huko UAE (muungano wa falme za kiarabu).

Gari hili lina uwezo wa kubeba askari wanne, dereva akiwamo. Limetengenezwa kwa teknolojia ambayo inalifanya haliwezi kupenyezwa na risasi hata ktk vioo vyake. Pia lina teknolojia ya kisasa kabisa inayoweza kutambua Bomu lililotegwa ardhini mita 100 kutoka linapoelekea au pembeni yake. Hivyo kumfanya dereva kukwepa kukanyaga Bomu hilo.

Hapo juu katika paa lake utaona mtutu wa Heavy Machine Gun(HMG) ambapo 12.7mm rounds huweza tumika, mtutu huo unatumia remote control. Pia linajilinda lenyewe kwa kuwa na uwezo wa kufyatua "smoke grenades" 8 kwa mpigo au guruneti maalum zinazotoa moshi mzito sana unaoziba eneo kubwa kwa haraka sana, na hivyo kumfanya dereva awakwepe washambuliaji wake kwa kuhama eneo alilokuwepo kwa haraka.

Majaribio yake yamekuwa yakifanyika huko Afghanistan, Iraq na mpakani mwa Pakistan na India, eneo la Kashmir.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages