JE UNAFAHAMU MADHUMUNI YA USAJILI WA VYOMBO VYA MOTO? - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, March 30, 2017

JE UNAFAHAMU MADHUMUNI YA USAJILI WA VYOMBO VYA MOTO?





Kwa watu wengi, uelewa wao juu ya madhumuni ya usajili wa vyombo vya moto unaishia kwenye kukusanya mapato. Ukweli ni kwamba, pamoja na hilo kuwa ni moja kati ya madhumuni ya usajili wa vyombo vya moto, bado kuna madhumuni mengine mengi ya usajili wa vyombo vya moto kama vile; kuonesha uhalali wa umiliki wa chombo husika, ndio maana kadi ya umiliki wa chombo husika hutolewa baada ya usajili.

Lakini pia usajili wa vyombo vya moto una dhumuni la kuonesha matumizi ya chombo kilichosajiliwa kwa maana kwamba kama chombo kimesajiliwa kwa matumizi *binafsi* ama kwa matumizi ya *biashara.*

Zaidi ya hayo usajili wa vyombo vya moto unadhumuni la kuonesha aina ya chombo, kama ni gari na ni gari la aina gani, ama ni pikipiki, trela, trekta mtambo, nakadhalika.

Dhumuni jingine la usajili wa vyombo vya moto ni kurahisisha uchunguzi wa uhalifu endapo utafanywa kuhusisha chombo cha moto. Lakini pia usajili wa vyombo vya moto hurahisisha utoaji wa taarifa mbalimbali zinazohusu vyombo vya moto kwa taasisi nyingine. (Information/Statistical data), mfano ajali za kugonga na kukimbia (Hit & Run accidents).

*Ndio maana Kifungu cha 8 (i) cha Sheria ya Usalama barabarani namba 30/1973 (CAP 168 RE.2002)* inaeleza kuwa hairuhusiwi kwa mtu yeyote *kuendesha chombo cha moto ambacho hakijasajiliwa.* Kipengele (2) cha sura hiyo hiyo kinaeleza adhabu kwa mtu atakayekamatwa akitumia chombo cha moto ambacho hakijasajiliwa kuwa ni pamoja na faini isiyozidi elfu hamsini za kitanzania au kifungo kisichozidi miaka mitano.

ANGALIZO HAPA NI KWAMBA: *Kumekuwa na taarifa za mitaani kuwa unaruhusiwa kutumia chombo cha moto kisichosajiliwa mpaka saa 12 jioni na siku za mwisho wa wiki na sikukuu.* Taarifa hizo sio sahihi, sheria inasema kwamba *hairuhusiwi kwa mtu yeyote kutumia chombo cha moto ambacho hakijasajiliwa.

Hapa juu nimetaja sheria ya usalama barabarani, Sheria ya Usalama Barabarani namba 30/1973 (CAP 168 RE.2002). Lakini si sheria hiyo pekee inayosimamia usajili wa vyombo vya moto. Kuna sheria nyingine kama vile, Sheria ya Usajili na Ubadilishaji wa Umiliki wa gari ya mwaka 1972. (Motor Vehicles Tax on Registration and Transfer Act of 1972). *Hivyo kununua chombo cha moto chenye usajili wa mtu mwingine na kukitumia bila kubadilisha umiliki ni kosa kisheria.* Hata hivyo kosa hili linaonekana ni la kawaida sana kwa jamii hasa kutokana na ugumu wa maisha na watu wengi kushindwa kununua magari mapya na hivyo kulazimisha kununua magari mikononi mwa watu wengine yakiwa tayari yalisajiliwa kwa matumizi yao.

*Sheria inamtaka kila mmoja kubadili umiliki mara baada ya kununua.*

Pia kuna kanuni mbalimbali za usalama barabarani zilizoundwa chini ya sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.

Moja wapo ikiwa ni Road Traffic Motor Vehicle Registration 2001. Sheria zote hizi zina lenga kuhakikisha kuwa kila mmoja anafuata taratibu sahihi za matumizi ya vyombo vya moto.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages