Saturday, March 25, 2017

TUMIA KALENDA YA UTE KUKWEPA MIMBA ZISIZOTARAJIWA NA KUPANGA MTOTO UMTAKAE
Kama mzunguko wa mwanamke ni kigeugeu yaani mwezi huu
28 mara 30 au 32 ama unaenda siku tatu, nne, tano au hata sita kwa vipindi
tofauti, basi itakuwa vigumu kwa mwanamke kukwepa kupata mimba kwa kusoma
kalenda.
Njia sahihi ni ya kusoma ute (kipindi cha
joto). Ndiyo maana wanyama kama ng'ombe, mbuzi na wengineo, kila
wanapojamiana kinachofuata huwa ni mimba tu, wao hutumia kalenda ya ute wa
uzazi.
Kwa mwanadamu kuna aina tatu za ute muhimu, zikizidi
tatu yaweza kukawa na maambukizi.
Ute Wa kwanza ni ute mweupe mzito, huu sio ute wa
uzazi kwa kipindi chochote utakapo onekana. Kwani unazuia mbegu za baba
kulifikia yai. Ute huu huua mbegu za baba ndani ya dakika 30 hivyo aina hii ya
ute haina uzazi.
Ute mwepesi, huu ni ute ambao tunauita "subiri
kidogo" maana yawezekana ukawa umetokana na mihangaiko ya mama kukasirika,
kuchoshwa, kuumwa homa au ikawa ni dalili ya yai kukomaa. Hivyo ukiuona ute huu
subiri siku moja uone kama ute utakata au kuongezeka.
Iwapo ute huu utaendelea kwa Siku mbili hadi tatu jua
hapo kuna uzazi. Lakini atakaye tungwa ni mtoto Wa kike. Hivyo kama lengo ni
kukwepa mimba usifanye tendo la ndoa.
Iwapo utapenda mtoto Wa kiume; Subiri kuanzia hapo
kwenye ute mwepesi mpaka "ute unaoteleza kama kiini cha yai". Ute huu
una uzazi asilimia 98 na unalenga kutungisha mtoto Wa kiume asilimia 99.
Hivyo basi kama wewe siku zako hazigandi, jifunze
kalenda ya ute na itakusaidia kupata mimba kwa kila tendo la ndoa
utakalolifanya. Na itakusaidia kuchagua ni mtoto wa aina gani unamuhitaji.
Kadhalika itakusaidia kukwepa mimba usiyoihitaji.
Kalenda ya mzunguko wa tarehe wengi wameshindwa kuitambua vyema kwa sababu ya
kubadilika badilika kwa siku zao zao hedhi kutokana na mikikimikiki ya maisha
ambapo iwapo mama atasafiri safari ndefu tu bila kujali umbali wa safari, siku
zake za hedhi zinaweza kuongezeka au kupungua.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Girls must be protected against FGM
Older Article
TAMTHILIYA YA KICHINA YA 'MFALME KIMA' ILIYOTAFSIRIWA KISWAHILI YAZINDULIWA NCHINI.
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MAKOREMO-MGONGORO
Hassani MakeroMar 12, 2025"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Hassani MakeroMar 12, 2025HALMASHAURI KUU YA CCM YAPENDEKEZA MAREKEBISHO YA KANUNI ZA UTEUZI WA WAGOMBEA UONGOZI
Hassani MakeroMar 11, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment