Friday, May 19, 2017

'Kazi yake Mola' nilituliza kichwa - Madee
Madee
Seneda amefunguka na kudai siri ya wimbo wa kazi yake mola kufanya vizuri mpaka
sasa ni kutokana na kutuliza kichwa wakati anaandika mashahiri yake tofauti na
vijana wa sasa ambao wanaingia studio wakiwa hawajui wanataka kuimba nini.
Jana
akiwa kwenye Planet Bongo ya East Africa radio, Madee amesema kuwa pamoja na
kuwa zimeimbwa nyimbo nyingi zenye mahadhi ya maombolezo lakini 'Kazi yake
Mola' bado imeendelea kuwa wimbo bora kutoka na
mashahiri kupangiliwa kwa ubunifu wa hali juu ikiwa ni pamoja na 'beat' ya P.
Funk Majani.
"Kazi yake Mola P. Funk aliitengenezea beat ambalo mpaka
sasa limeweza kudumu, lakini pia mashairi niliyaandika kwa umakini mkubwa kwani
ndo nilikuwa nimepatiwa nafasi ya kuonyesha uwezo wangu. Japo wimbo haukuwa wa
kutoka officially lakini nilijitahidi kuandika mashairi yenye maudhui, ndio
maana mpaka sasa wimbo unaonekana hit.
Vijana wa sasa wameshindwa kutoa nyimbo itakayoizidi 'kazi yake
mola' kwani wengine mpaka wanaingia studio hawana hata mashairi wanataka
wasikie mdundo ndio wapate kitu cha kusema"- Madee.
Aidha Madee ameongeza kutokana na ubora wa kazi yake mola
amewaomba mashabiki zake kuendelee kuutumia katika maombolezo ya ndugu, jamaa
na marafiki akiwepo Msanii aliyetamba na wimbo ya Kazi yangu ya dukani, Dogo
Mfaume aliyefariki dunia mapema jana.
Tags
# BURUDANI
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Zlatan Ibrahimovic kwenye mapumziko mjini Miami nchini Marekani
Older Article
BOLLYWOOD WAMPATA RAMBO WA KIHINDI
RAIS MWINYI: ASANTENI WASANII WOTE KWA KUNIUNGA MKONO
Hassani MakeroJan 24, 2025Light Upon Light Summit in Zanzibar Set to Inspire and Unite Global Muslim Community12th & 13th October 2024.
kilole mzeeSept 30, 2024BENDI ZA MUZIKI WA DANSI KUWASHA MOTO TAMASHA LA USIKU WA WAFIA DANSI JIJINI DAR ES SALAAM
Hassani MakeroMay 12, 2022
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment