Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni kizimbani kwa rushwa - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, June 20, 2017

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni kizimbani kwa rushwa


Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni na mfanyabiashara wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka manne ya kuomba na kupokea rushwa.

Mwendesha Mashtaka kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Emmanuel Jacob amewataja washtakiwa hao kuwa ni  Omary Mohammed Abdallah ambaye ni Hakimu na mfanyabiashara George Joseph Barongo.

Wakisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Respicious Mwijage, imedaiwa kuwa, kati ya January na Februari 12/ 2017 hakimu Omary alitenda kosa.

Imedaiwa kuwa, siku hiyo Omary akiwa muajiriwa wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni aliiomba rushwa  ya sh. 205,000 kutoka kwa Agnes Nyenza kwa ajili ya kumsaidia kwenye kesi yake ya mirathi ya namba 570/2016 ambayo ilikuwa mbele yake.

Katika shtaka la pili Hakimu Omary anadaiwa kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha Kutoka kwa Nyenza ili aweze kumsaidia katika kesi hiyo.

Mahakama imeendelea kuambiwa kuwa, kati ya Februari na Machi mwaka huu, jijini Dar es salaam, Hakimu Omary akiwa na mfanyabiashara Barongo waliomba rushwa ya sh. Milioni moja kutoka kwa Nyenza kwa ajili ya kumsaidia katika kesi hiyo ya mirathi.

Wakili wa Takukuru aliendelea kuieleza mahakama kuwa, siku na mahali hapo watuhumiwa hao wote kwa pamoja walipokea rushwa ya sh. 500,000 kwa ajili ya kumsaidia Agnes Nyenza kwenye kesi yake ya mirathi ambayo iko mbele ya hakimu huyo Omary Mohammed wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wako nje kwa dhamana hadi Julai 4 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages