Taasisi ya kuzuia na kupambana Rushwa
nchini (TAKUKURU), imewafikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu watu wawili
James Rugemalira (Pichani kushoto) na Harbinder Seth Sigh (Pichani kulia) kwa
tuhuma ya kesi ya Uhujumu Uchumi.
Akizungumza mapema jana
mchana jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kupambana na Kuzuia
Rushwa nchini (TAKUKURU), Valentino Mlowola amesema kuwa Mmiliki wa VIP
Engineering and Marketing, James Rugemalila na Mmiliki wa Kampuni ya IPTL,
Harbinder Seth Sigh wamefikishwa mahakama ya Kisutu jana mchana kwa kosa la
kuhujumu uchumi pamoja na makosa mengine yanayofanana na hayo.
Mlowola amesema kuwa
watuhumiwa hao wameshafikishwa mahakamani kwa kosa la kuhujumu uchumi pamoja na
makosa yanayofanana na hayo, akaongeza kusema kuwa TAKUKURU wamechunguza shauri
hilo kwa muda mrefu na sasa imefika wakati kuwapeleka mahakamani watuhumiwa hao
kujibu mashtaka yao.
Mlowola ametoa Wito kwa
wananchi kutambua kuwa serikali ina nia njema na dhati kabisa ya kuwapa Maisha
bora Watanzania, hivyo hakuna budi wale wote wanaotuhumiwa kwa makosa mbali
mbali watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Kabla ya vigogo hawa
wawili kufikishwa mahakamani jana, baadhi ya watumishi wa TANESCO tayari
walishtakiwa kufuatia tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni
ya VIP Engeneering and Marketing ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya
kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.
Mmiliki
wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemalila na Mmiliki wa Kampuni ya
IPTL, Harbinder Seth Sigh wakiwa wamechuchumaa kabla ya kupelekwa kwenye chumba
cha mahakama kwa ajili ya kusomewa mashitaka yao,likiwemo la Uhujumu uchumi
Mmiliki
wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemalila na Mmiliki wa Kampuni ya
IPTL, Harbinder Seth Sigh wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu tayari kwa kusomewa mashitaka yao,likiwemo la Uhujumu uchumi.
No comments:
Post a Comment