Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ameachiwa kwa dhamana baada ya
kuhojiwa kwa saa nne katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
(DCI).
Lowassa ameondoka makao makuu ya polisi saa 8.15 na kuelekea nyumbani kwake.
Akizungumza baada ya mahojiano hayo, Mwanasheria wa Chadema, Peter
Kibatala amesema Lowassa amejidhamini mwenyewe na ametakiwa kuripoti tena
Alhamisi saa 6.00 mchana.
Kibatala amesema Lowassa amehojiwa kwa kosa la uchochezi na ameandika
maelezo ya onyo juu ya kauli aliyoitoa wakati wa futari iliyoandaliwa na mbunge
wa Ukonga, Mwita Waitara.
"Mzee amehojiwa kwa kile wanachokiita kauli ya uchochezi aliyoitoa
Juni 23, mwaka huu wakati wa futari iliyoandaliwa na Waitara. Baada ya kuhojiwa
ameandika Maelezo ya Onyo na atatakiwa kuripoti tena Alhamisi, Juni 29,"
amesema.
No comments:
Post a Comment