WATEJA 2000 WA AIRTEL WAJINYAKULIA ZAWADI. - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Wednesday, February 7, 2018

demo-image

WATEJA 2000 WA AIRTEL WAJINYAKULIA ZAWADI.

01
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati wakuchezesha droo ya kwanza ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ambapo washindi 2000 kila mmoja alijishindia 1GB. Kushoto ni ni Msimamizi  kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah Hemedy na Afisa Masoko wa Airtel Nassoro Abubakar. (Picha na Brian Peter)
Promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti ilizinduliwa mapema wiki hii ambapo kuna washindi 1,000 wakila siku ambao wanajishindia bando ya 1GB pamoja na zawadi nyingine kemkem zikiwepo simu za kisasa za smatiphone na modem za kisasa.
Akiongea baada ya droo hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema wateja 2000  wa Airtel wameweza kujishindia bando ya 1GB. 
Kama mnvyoona hapa leo droo ya promosheni yetu ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti imefanyika leo kwa uwazi na washindi wetu wameweza kutoa shukrani na kutuhakikishia kuwa wataendelea kutumia mtandao wetu makini na bora  wa Airtel, alisema Mmbando.
Ni muhimu kufahamu kuwa mteja haitaji kujisajili kwa ajili ya promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti. Kile anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*99# halafu chagua namba 5 Yatosha SMATIKA Intaneti, hapo utanunua bando aidha ya siku, wiki au mwezi na kuwa mmoja wa washindi wa zawadi zetu kabambe, aliongeza Mmbando.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *