Sijawahi Kunyakua Bwana Wa Mtu- Thea - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Thursday, May 10, 2018

demo-image

Sijawahi Kunyakua Bwana Wa Mtu- Thea

0FD38C98-2432-43CE-96B2-CFBF8A406B0F

Msanii mkongwe wa Bongo movie Salome Urassa maarufu kwa Jina la usanii kama Thea, amefunguka na kuweka wazi kuwa katika maisha yake hajawahi hata siku moja kunyakua bwana wa mtu.

Watu maarufu hasa Kwenye tasnia ya Bongo fleva na Bongo movie wamekuwa wakinyosheana vidole na kutuhumiana kwa vitendo vya kuchukuliana mabwana au wanaume.

Kwenye mahojiano  na Mwandishi wetu, Thea aliweka wazi kuwa, suala la kuibiana mabwana halipo kwa wasanii tu, bali ni kwa jamii nzima, lakini kwa upande wake hajawahi  kumzunguka mtu kwa kuwa hiyo ni tabia ya mtu na kwake haipo.

"Kiukweli  tangu niyajue mapenzi, sijawahi kuiba bwana wa mtu kwasababu siyo tabia yangu na siwezi kufanya hivyo, wanaochukua mabwana za watu ni tabia zao ambazo huwezi kuzibadilisha na hii haipo kwa wasanii tu, bali ni kwa jamii kwa jumla kwani tumekuwa tukisikia sana ila kwa wasanii wanaonekana zaidi kutokana na majina waliyonayo”.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *