BENKI YA NBC YACHANGIA UJENZI WA KITUO CHA POLISI RUANGWA MKOANI LINDI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, February 15, 2019

BENKI YA NBC YACHANGIA UJENZI WA KITUO CHA POLISI RUANGWA MKOANI LINDI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto), mara baada ya kupokea msaada wa mifuko 1000 ya saruji kutoka NBC, kwa ajili ya ujenzi wa kituo  cha polisi cha Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi. Wengine kutoka kushoto ni, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Neema Singo, Meneja Mahusiano, William Kallaghe, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Flora Molel na Mkurugenzi wa Kitengo cha Malalamiko, Sarah Laiser.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (wa pili kushoto), akipokea mfano wa hundi ya shs 11,270,000 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, kwa ajili ya kununulia mifuko 1000 ya saruji kama  mchango wa NBC kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi cha Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi. Hafla ya makabidhiano  iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

BENKI ya NBC imetoa msaada wa mifuko 1000 ya saruji kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi cha Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Msaada huo umekabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa katika ofisi zake Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi anasema  NBC ni Benki ya Wazalendo na tunajiona fahari kuweka juhudi zetu katika kuhakikisha kila mwananchi na mzalendo waTaifa letu anaishi kwa usalama na utulivu.

“Kama taasisi ya fedha ni imani yetu kuwa Jeshi la Polisi likiwezeshwa kwa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo majengo ya vituo pamoja na makazi ya askari litaweza kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa ufanisi ambayo ni kulinda usalama wa raia na mali zao.

Benki ya NBC inajua pia eneo litakalojengwa kituo hiki wapo wateja wetu na wale wateja watarajiwa hivyo ujenzi wa kituo hiki utasaidia sana kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo hivyo kuwafanya wakazi wake kuzalisha mali katika hali ya utulivu hiyvo kukuza uchumi wao na wa Taifa.

“Benki ya NBC inapenda kutoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais John  Pombe Joseph Magufuli kwa jitihada zake katika kujenga mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili kwa pamoja kutimiza azma ya kuelekea Tanzania ya viwanda.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages