Uber yazindua bima ya Ulinzi dhidi ya Majeraha kwa madereva na abiria nchini Tanzania bila gharama yoyote ya ziada - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, February 18, 2019

Uber yazindua bima ya Ulinzi dhidi ya Majeraha kwa madereva na abiria nchini Tanzania bila gharama yoyote ya ziada


Madereva na abiria wa Uber nchini Tanzania watakuwa na amani zaidi wakitumia Uber, kwa kuwa Uber imetangaza kuzindua bima ya Ulinzi dhidi ya Majeraha, inayotolewa na UAP Old Mutual. Tangazo hili ni sehemu ya ahadi kuu ya Uber katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika (MEA) na ni suluhisho la kipekee, la kwanza kwa madereva na abiria linalotumia programu za teknolojia nchini Tanzania.

Madereva wote wa Uber, pamoja na madereva wa uberPOA watafaidika na bima hii bunifu bila gharama yoyote ya ziada; kuanzia wakati unapokubali safari, wakati unaendesha gari kumchukua abiria, na hadi wakati safari inapokamilika. Bima ya abiria itawashughulikia kuanzia wakati safari zao zinapoanza, hadi mwisho wa safari.

Katika tukio la bahati mbaya la ajali au tukio linalohusiana na uhalifu na kusababisha majeraha wakati wa safari, abiria na madereva wataweza kupata faida zifuatazo:

  • Bima ya matibabu: Ikiwa ajali itatokea Wakati wa Safari, bima hii itawafidia madereva na abiria kwa gharama husika za matibabu hadi TZS 1 250 000. Kwa kuongezea, bima hii hufidia gharama za huduma ya ambulensi.
  • Malipo ya kifo na mazishi: Katika tukio la bahati mbaya ambapo dereva au abiria anaaga dunia kama matokeo ya ajali Wakati wa Safari, watu wanaomtegemea au warithi watafaidika na malipo ya pesa taslimu ya TZS 5 000 000. Watapata pia kiasi cha TZS 500 000 cha gharama za mazishi.
  • Malipo ya kulemazwa kabisa: Katika tukio la bahati mbaya ambapo dereva au abiria amelemazwa kabisa kama matokeo ya ajali Wakati wa Safari, watafaidika na malipo ya pesa taslimu ya TZS 5 000 000. Kiasi kinategemea na hali ya ulemavu, kama iliyobainishwa na UAP Old Mutual.
  • Faida ya malipo ya kila siku kwa madereva (majeraha): Ikiwa dereva amelazwa kwa zaidi ya saa 48 kama matokeo ya ajali ambayo ilifanyika Wakati wa Safari hivyo basi hawezi kuendelea kuendesha gari kwa sababu ya majeraha hayo, atapokea malipo ya kila siku ya TZS 10 000 hadi siku 30 ikiwa amethibitishwa na daktari kuwa hafai kufanya kazi.

Akitoa maoni yake kuhusu ushirikiano huu, Alfred Msemo, Mkuu wa Uber nchini Tanzania alielezea, “Tunaamini ushirikiano huu na UAP Old Mutual utahusika pakubwa katika kufanikisha lengo letu la chaguo thabiti, la bei nafuu, na salama la usafiri kwa Watanzania wote. Tutaendelea kuchukua maoni kutoka kwa watumiaji wetu wote ili kuhakikisha tunaboresha zaidi uzoefu wao ili waweze kutumia Uber kwa ujasiri zaidi”.  

Damas Filied, UAP Old Mutual Life Assurance, “Kama biashara kuu ya Afrika tunagundua kwamba tunajukumu kubwa, tukishirikiana na washikadau wengine kuwaunga mkono wateja wetu kwa kulinda kile ambacho ni muhimu kwao. Toleo hili la bidhaa bunifu, ni mfano mwema wa hilo, na tunatazamia ushirikiano wa muda mrefu unaofaidi pande zote.”

Sera ya Ulinzi dhidi ya Majeraha, ambayo itaanza kutumika tarehe 21 Desemba 2018, imetengenezwa hasa kwa madereva wale walio barabarani na kwa abiria wanaohitaji chaguo salama, thabiti na la bei nafuu la kuzunguka katika mji wao. Uber inaendelea kuimarisha usalama unaopatikana kupitia programu ya Uber na kuhakikisha safari salama wakati wa kila safari iliyopatikana kupitia programu ya Uber. Hivi karibuni Uber ilizindua Zana ya Usalama yenye vipengele vipya kama vile Kituo cha Usalama na Watu Unaowaamini kwa abiria na taarifa inayoweza kugeuzwa kukufaa ya kasi na kitufe cha dharura cha dereva ambacho huwaunganisha madereva moja kwa moja kwa makampuni binafsi ya usalama yakihitajika kupitia mtoa huduma mwingine.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages