Mwanamfalme wa Saudia akanusha madai ya kuinunua Manchester United - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, February 18, 2019

Mwanamfalme wa Saudia akanusha madai ya kuinunua Manchester United



Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman amekanusha madai kuwa anantaka kuinunua Manchester United kwa kitita cha pauni bilioni 3.8.

Tetesi ziliibuka mwishoni mwa wiki zikimuhusisha mwanamfalme huyo na kutaka kuinunua klabu hiyo tajiri nchini Uingereza.

Wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazers wanadaiwa kuwa hawana mpango wa kuiuza timu yao.

Wamiliki hao kutoka Marekani waliinunua Man United kwa kitita cha pauni milioni 790 mwezi Mei 2005.

"Ripoti zinazomuhusisha Mwana Mfalme Mohammed Bin Salman kuwa anataka kuinunua Manchester United ni uongo mtupu," amesema waziri wa michezo wa Saudia Turki al-Shabanah.

"Manchester United walifanya mkutano na mfuko wa uwekezaji wa umma PIF wa Saudia kuhusu nafasi ya udhamini. Lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa," ameeleza waziri huyo.

Salman, 33, aliteuliwa kuwa mrithi wa kiti cha Ufalme wa Saudia Juni 2017.

Chini ya utawala wake, taifa hilo limelaaniwa vikali kwa visa vya kukiuka haki za binaadamu na kushutumiwa kwa mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi katika ubalozi wa Saudia nchini uturuki mwaka jana.

Mwezi Oktoba mwaka jana, Manchester United ilijitoa kwenye mazungumzo na PIF baada ya mauaji ya Khashoggi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages