Wananchi Mkoani Arusha,
wametakiwa kujitolea kwa mali na vitu walivyonavyo kwa ajili ya kumtumikia
Mungu ili waendelee kubarikiwa.
Rai hiyo, ilitolewa na
Mbunge viti Maalum wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Amina Mollel, wakati wa
harambee ya umaliziaji wa jengo la Ibada katika Kanisa Katoliki Kigango cha
Lengijave wilayani Arumeru, mkoani hapa.
Katika harambee hiyo jumla
ya Sh. milioni 100, zilikuwa zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo
ya ibada.
Viongozi wengine
walioshiriki katika harambee hiyo ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, William Ole Nasha na baadhi ya viongozi wa dini kutoka maeneo
mbalimbali ya Mkoa wa Arusha.
Katika harambe hiyo, Jumla
ya Sh. milioni 14 zilipatikana ahadi ikiwa ni Sh. millioni 7.
No comments:
Post a Comment