Kampeni ya Matibabu ya
Upasuaji wa Moyo kwa Watoto 10 kila mwezi kwa muda wa miezi Sita kutoka familia
duni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda
imeendelea kuwa na mafanikio makubwa ambapo Balozi wa Jumuiya ya Falme za
Kiarabu UAE Bw.Khalfan Abdulrahman Al-Mazouqi amemuunga mkono kwa kuleta
madaktari bingwa wa kufanya upasuaji kwa watoto hao.
RC Makonda amesema Balozi
huyo ameamua kujitolea Madaktari hao baada ya kuona kipande cha Video
kikimuonyesha RC Makonda akiwa yupo kwenye wodi ya watoto wenye matatizo ya
moyo kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya jambo lililomgusa balozi na kuamua
kumuunga mkono kwenye kampeni hiyo.
Aidha RC Makonda amesema kuwa
hadi sasa jumla ya watoto 30 kati ya 60 wamefanyiwa upasuaji kwa kipindi cha
miezi mitatu huku akitoa wito kwa wananchi na wadau kugusa maisha ya wenye
uhitaji kwa kuwafika taasisi ya moyo Jakaya Kikwete na Kujitolea kugharamia
upasuaji kwa watoto kwahuwa hadi sasa kuna zaidi ya watoto 500 wenye tatizo la
moyo lakini wazazi hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akifurahi pamoja na mmoja wa watoto wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) wakati wa hafla ya kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Kutoka kulia ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Prof. Mohamed Janabi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, Kiongozi kutoka shirika la Sharjah Charity Group Ali Mohamed Alrasholi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakimsikiliza Daktari kutoka Shirika la Sharjah Charity Group wakati wa hafla ya kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akifurahi pamoja na mmoja wa watoto wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) wakati wa hafla ya kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akitenda jambo kwa viongozi hao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akifurahi pamoja na mmoja wa watoto wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) wakati wa hafla ya kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kuhitimisha kambi maalumu ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika picha ya pamoja na wataalamu wa afya, viongozi mbalimbali na watoto wenye magonjwa ya moyo wanaopata matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam. Kulia kwa waziri ni Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akifurahi pamoja na mmoja wa watoto wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) wakati wa hafla ya kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati), Balozi wa Falme za Kiarabu Mhe. Abdulrahman Mohamed Marzooqi (kulia) pamoja na Kiongozi kutoka shirika la Sharjah Charity Group Ali Mohamed Alrasholi wakimpatia zawadi mtoto mwenye magonjwa ya moyo anayepata matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kuhitimisha kambi maalum ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Sharjah Charity Group leo Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment