Nabii Suguye wa Kanisa la WRM, Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga, Dar es Salaam |
Wakazi wa jiji la Dar es
Salaam nan je ya jiji hilo wanaohudhuria Ibada ya mbalimbali kanisani WRM
lililopo Kivule Matembele ya Pili, Ukonga chini ya uongozi wake Nabii Nicolaus
Suguye wamezidi kupokea miujiza yao kutoka kwa Mungu baada ya kusumbuliwa na
maradhi kwa miaka mingi bila kupona.
Nabii Suguye amekuwa msaada
kwa wengi waliopata neema ya kuhudhuria Ibada Kanisani hapo;
Eliza Mwita binti aliyezaliwa
akiwa kipofu alipataneema ya kuombewa na Nabii, kama maandiko yasemavyo “……wataweka mikono yao juu ya wagonjwa,
nao watapata afya.” (Marko 16:18)
Eliza aliweza kuona papo hapo.
Matilda Mhelela
naye alikuwa na changamoto ya kuona kwa takribani mwaka mmoja, japo aliweza
kutembelea hospitali nyingi kwaajili ya matibabu bila ya mafanikio, lakini kwa
neema alipohudhuria ibada ya maombezi iliyoongozwa na Nabii Nicolausi Suguye,
na kupita katika kisima cha Baraka na Uponyaji, shida yake ilikoma pale pale na
sasa anaona kama kawaida.
Bi Cesilia Gulasa ambaye
hakuweza kuitambua miaka yake kutokana na uzee, aliponywa ugonjwa wa moyo
uliokuwa unamsumbua kwa miaka mitano huku akimaliza kila aina tiba bila
mafanikio. Bibi huyo anasema usiku alikuwa halali kutokana na maumivu makali
aliyokuwa akiyapata.
Mmoja wa wenye changamoto wanao hudhuria kanisani hapo kupokea miujiza yao |
Mbali na hao watu wengine ambao Mungu aliamua kuwaponya na kujitukuza kupitia Mtumishi wake Nabii Nicolaus Suguye ni Justine Mahoka ambaye alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya mguu kwa muda mrefu na kupelekea ashindwe kutembea kutokana na mguu huo kuoza na kutoa harufu kali, alijikuta anatembea kama kawaida baada ya kufanyiwa maombi na Nabii Suguye kanisani hapo.
Naye baba mmoja aliyejulikana kwa jina moja,
alijikuta anapona vidonda vya tumbo ambavyo vilikuwa vinamsumbua kila nyakati nyakati
za usiku, na kutumia kila aina ya dawa bila mafanikio huku akipinga uweza wa
Mungu kama anaweza kupona ugonjwa huo. Akisimuliwa mkasa huo kwa
niaba ya mumewe, Maria Sande alisema kuwa mumewe kwa muda mrefu alikuwa
anakaidi kwenda katika makanisa ya Kiroho kutokana na kukumbatia dini yake,
hata hivyo baada ya kuzidiwa na ugonjwa huo aliomba apelekwe katika huduma hiyo
kwenda kuombewa baada ya kusikia kuwa watu wengi wenye magonjwa yaliyoshindikana
kibinadamu wanaponywa kwa uwezo wa Mungu.
“Yaani kweli Suguye ni Nabii wa Mungu, maana
kuna vitu unaweza kusema ni maigizo lakini sio yanayotendeka pale kanisani, kwa
macho yangu; kuna binti alikuwa anatumikishwa mambo ya kichawi anaitwa Bahati,
wakati wa maombezi nilimuona akisukwa sukwa nikadhani anataka kutapika kama
ilivyokawaida pale kanisani, kama ulishawahi kulishwa vitu vibaya kwa hali ya
kawaida au ulimwengu war oho utavitapika tu na kuwa salama, basi binti Yule
ajabu ya Mungu wa Suguye, alianza kutoka damu mdomoni, nikaogopa, haaa! Akaanza
kutapika wembe, ajabu, na sio wembe tu, akatapika mkufu! Mwishowe akatapika
sindano! Huyu Mungu wa Suguye ni noma” Alisikika Bi Fidea Hiza kutoka Dodoma,
alipohojiwa na mwandishi wetu.
Naye Hasani Dunia kutoka Ambanguru Tanga;
alidiriki kumuita Suguye ni kama Gurdiola mkufunzi wa timu ya Manchester City
ya Uingereza; “Aaah! Suguye mchawi kama Gurdiola, yaani pale mnaposema hii kitu
haiwezekani, ndipo upako wake unapowafurahisha, Suguye kama ni mchawi basi yeye
ni kiboko yao, kiukweli Mungu anamtumia ipasavyo, na katika namna ya ajabu”
Mmoja wa wenye changamoto akipokea uponyaji wake |
Mara kadhaa Nabii Suguye katika mahojiano
mbalimbali na WRM TV husema kuwa watu wengi wamekuwa wakibeza miujiza
inayotendeka katika huduma zinazotolewa na watumishi waliopakwa mafuta na
Mungu, na kujikuta wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji hali ambayo
huwasababishia kupoteza fedha nyingi kwa kuwapa waganga hao huku wakikimbia
huduma inayotolewa bure na Mungu.
Nabii Suguye kupitia Ibada mbalimbali
zifanyikazo kanisani WRM Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga, jijini Dar es
Salaam; amekuwa msaada mkubwa kwa watu mbalimbali wanaopata neema ya
kuhudhuria, kwani wenye changamoto mbalimbali za afya wanapokea uponyaji wao;
wenye changamoto za uzazi na uchumi, wanashuhudia kupokea Baraka zao, hakika
Mungu wa mahala hapa huwaudumia wote wajao kwa moyo thabiti bila kuangalia
dini, dhehebu, kabila au ukubwa wa changamoto yako.
No comments:
Post a Comment