Na Sosthenes Makero, WRM
MKUU wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa anawashangaa viongozi na watu wanao
mshangaa wakiziona picha zinazozagaa mitandaoni akilia madhabahuni; “Naomba
niwaambie kitu, neno hili mnalojifunza hapa nibora kuliko kitu chochote,
ninawashangaa wale wanaonishangaa nikilia madhabahuni; labda niwaambie vizuri,
ni bora mimi ninayelia madhabahuni kumlilia Mungu anishindiaye vita kuliko Yule
aliliaye mapenzi huko mtaani”
Hatua hiyo ya
Makonda kusema maneno hayo baada ya kubaini watu wengi siku hizi hawaishi
katika kumtegemea Mungu, maana watumishi wa Mungu wanajitahidi kuifundisha
jamii yetu kukiri ushindi kupitia neno la Mungu, lakini jamii hii inapotokea
changamoto kidogo katika maisha yao ya kila siku humsahau Mungu na kujikuta
wakitafuta njia mbadala kutatua changamoto iliyo mbele yake.
“Mwanafunzi
anapoingia chuo akasomea udaktari, anapomaliza miaka yake minne au mitano
akaajiriwa Muhimbili anachokifanya pale, ni kuutumia ule ujuzi, ule ufahamu
alioupata kwa miaka yake mitano darasani, na kuutumia maabara, katika hali ya
kutaka kufanya kipimo cha kugundua kama huyo mgonjwa ana malaria au la;
anachokifanya ni kusoma, taarifa anayoipata maabara na kuoanisha na taarifa
aliyoisoma darasani na mwisho ana hitimisha huyu ni mgonjwa wa malaria au la!”
“Tofauti na sisi
wakristo wa leo, tunapoingia kwenye majaribu, tunasahau darasa tunalofundishwa
na ‘Prophet’ tunaiweka biblia pembeni, neno la Mungu pembeni, tunataka kuingiza
ujuzi mpya tofouti na mafundisho tuliyoyapata kanisani, ndio maana tunafika
mahali tunalia kuwa Bwana ametuacha na wakati hajawahi kutuacha, maandiko
yanasema; Kwa kuwa Bwana
hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzao wa
wasio haki ataharibiwa (Zaburi 37:28) tunapoingia kwenye majaribu tunasahau
yakwamba huyu niliyemuomba jumapili ndiye aliyenifikisha hapa, na ndiye ajuaye
kesho yangu, kumbuka unapoingia kwenye majaribu kaa kwenye neno la Mungu pekee,
Usikubali shetani akunyanyase”
Mhe. Makonda
aliyasema hayo yote alipokuwa akizungumza na waumini wa Kanisa la WRM, lililopo
Kivule Matembele ya Pili, Ukonga jijini humo linaloongozwa na mtumishi wa
Mungu, Nabii Nicolaus Suguye, jumapili iliyopita.
Makonda aliongeza
kuwa “Katika watu ambao wanapitia magumu, mimi ni mmoja wao; kama kuna mtu
alipingwa kwenye nafasi yake ya ukuu wa mkoa nipo, kama kuna mtu alipigwa kwa
kusemwa kwa habari ya ndoa yake kukosa motto mimi nipo, kama kuna mtu alipigwa
kutoka kwenye familia masikini nipo, kama kuna mtu niliyesoma kwa tabu, shida
na manyanyaso nipo, kwanini leo nisimshukuru Mungu wangu aliyenipa hivi
nilivyonavyo leo”
“Unamuoneaje haya
Mungu aliyekuumba, na kukupatia pumzi yake bure?” aliongeza.
Mkuu huyo alimpongeza
nabii Suguye kutumika sahihi kwa Kristo, maana ni watumishi wachache sana
wanaokumbuka kumjengea Mungu hekalu kwaajili ya wamuni kuabudia, wengi wao
huzitapanya sadaka wazikusanyazo kwaajili ya matumizi binafsi na si kwaajili ya
huduma.
RC Makonda ametaka
wakina mama wamshirikishe sana Mungu kwa maombi ya kumaanisha katika kutatua
changamoto za familia zao na si kukurupuka na kukimbilia kwa mahakamani au
mabaraza kwani hata hao wanaopelekewa wanachangamoto zao na familia zao,
yawezekana zao ni kubwa kuliko zako.
Aidha Makonda
amekiri kuzifahamu changamoto zinazolikabili Jimbo la ukonga hasa maeneo ya
kivule na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi wake; “Kiukweli nafahamu changamoto za
jimbo hili, najua kuna changamoto huduma ya uhakika ya afya, miundo mbinu
mibovu ya barabara hasa nyakati za masika, ukosefu wa maji salama ya kunywa,
usalama wa raia na mali zao, napenda kutumia madhabahu hii, kuwaahidi
nitalishughulikia”.
No comments:
Post a Comment