Waziri wa Ujenzi, na Mawasiliano,
Mhandisi Isack Kamwele (kushoto), akizungumza na MKurugenzi wa Biashara wa
Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (wa tatu kushoto), mara baada ya mkutano mkuu wa
mwaka wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), ambako benki hiyo
ilizindua rasmi huduma yake mpya ya mkopo wa bima. Wanaoangalia ni baadhi
ya maofisa wa benki hiyo.
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua
mkopo wa bima ikiwalenga zaidi wafanyabiashara walio katika sekta ya uchukuzi.
Akizungumza na washiriki wa mkutano mkuu wa
mwaka wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru alisema mkopo
huo unapatikana kwa kuanzia kiasi cha shilingi milioni 1 mpaka milioni 300.
Alisema mkopo wa bima wa NBC ni kwa ajili ya
bima za biashara zote zikiwemo biashara za magari, bidhaa zilizo safarini, majanga
ya moto, ujambazi, hatari zote za barabarani na ajali kwa wafanyakazi.
“Mtu yoyote mwenye mahitaji ya bima akiwa na
rasilimali zozote kama vile nyumba ana sifa ya kupata mkopo huu bila kuwa na
dhamana yoyote.
“Utalipia miezi miwili ya bima yako NBC na
sisi tutalipia miezi 10 inayobaki kwa wakala wa kwa niaba yako, nawe utailipa
benki kila mwezi kidogo kidogo. Mkopo huu una riba ndogo kabisa kuliko mikopo
yote inayotolewa na benki”, aliongeza Bwana Ndunguru.
Pamoja na hayo mkurugenzi huyo alisema,
uamuzi wa kuanzisha huduma inayowalenga wafanyabiashara imetokana na kasi ya
utendaji wa serikali ya awamu ya tano katika kuondoa kero zikizokuwa
zikiizorotesha sekta ya uchukuzi.
“NBC imeongeza kutoa mikopo zaidi katika
sekta ya usafirishaji, mkopo wa bima kutoka NBC unakuwezesha kuendelea kuikinga
biashara yako dhidi ya hasara au matatizo mengine yoyote hata kama huna fedha
taslimu za kulipia bima”, alisema.
Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa
Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwele alipongea NBC
katika juhudi inazofanya katika kuinua sekta ya biashara ndogo na za
Kati.
Akitoa mfano Waziri Kamwele alisema ni hivi
karibu Benki ya NBC ilisaini makubaliano na Shirika la Posta Tanzania ambapo
benki itaweka ofisi katika kila palipo na tawi la Shirika hilo popote nchini.
No comments:
Post a Comment