Monday, September 23, 2019

Home
KITAIFA
RC MAKONDA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA STAND MPYA YA MABASI MBEZI LUIS, AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI KABLA YA MAY 2020
RC MAKONDA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA STAND MPYA YA MABASI MBEZI LUIS, AMTAKA MKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI KABLA YA MAY 2020
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe. Paul Makonda leo September 23 ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi
wa Stand mpya ya kisasa ya Mabasi ya Mikoani na Nchi za Jirani ya Mbezi Luis
ambayo ujenzi wake umefikia 35% hadi sasa na Kumtaka Mkandarasi kukamilisha
Ujenzi huo kwa wakati.
RC Makonda amesema ujenzi wa
Stand hiyo utagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 50.9 ambapo ndani yake
kutakuwa na huduma zote muhimu ikiwemo Jengo la Abiria,Utawala, Maegesho ya
mabasi 500, Shopping Mall, Hotel, Maegesho ya Taxi, Bajaji, Pikipiki, Bank,
Petrol station, Apartment, ofisi za mabasi, sehemu ya wafanyabiashara, mama
Lishe,Vyoo, Kituo cha Polis na sehemu ya kuhifadhi mizigo.
Aidha RC Makonda amemuelekeza
katibu Tawala wa Mkoa huo kuunda Kamati ya kufuatilia Maslahi ya wafanyakazi
wote wanaofanya kazi katika miradi ya kimkakati ili kuhakikisha wanapata
stahiki zao zote ikiwemo mishahara na mifuko ya hifadhi ya jamii.
Pamoja na hayo RC Makonda
ameendelea kuwataka wakandarasi wa miradi mbalimbali kuhakikisha wananunua
vifaa kutoka kwenye Viwanda vya wazawa jambo litakalosaidia kuinua uchumi wa
Viwanda na Taifa kwa ujumla.
Katika Ziara hiyo RC Makonda
ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam
na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Benki ya Absa Tanzania na World Vision Tanzania Washirikiana Kuboresha Upatikanaji wa Maji katika Kijiji cha Kwedizinga
Hassani MakeroMar 19, 2025WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MAKOREMO-MGONGORO
Hassani MakeroMar 12, 2025"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank
Hassani MakeroMar 12, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment