Mkurugenzi Ushirika na Uwajibikaji wa Jamii EMEA na Mkuu wa wiki
ya Code Afrika, Claire Gillissen (kulia), akizungumza na Walimu kutoka shule
mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kutoa mafunzo ya Programming kwa walimu kutoka Tanzania na Afrika nzima yenyelengo la kukuza elimu mashuleni na na jamii nzima. uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa SAP, Liam Ryan, akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa uzinduzi wa kutoa mafunzo ya Programming kwa walimu kutoka Tanzania na Afrika nzima yenyelengo la kukuza elimu mashuleni na na jamii. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Miradi wa taasisi ya Apps and Girls, Jesca Mmari,
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kutoa mafunzo ya Programming kwa walimu kutoka Tanzania na Afrika nzima yenyelengo la kukuza elimu mashuleni na na jamii. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwalimu wa shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa akizungumza katika haflahiyo.
Kutokana na umuhimu wa teknolojia katika elimu na jamii
kiujumla kuongezeka,Kutokana na umuhimu wa teknolojia katika elimu na jamii
kiujumla kuongezeka,Taasisi ya SAP kupitia program ya INITIATIVE CODE WEEKS
imeanza kutoa mafunzo ya Programming kwa walimu kutoka
Tanzania na Afrika nzima kwa lengo la kuwafikia wanafunzi wengi na kutengeneza
msingi mzuri wa teknolojia kwa kizazi cha baadae.
Akizungumza
leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa
SAP, Liam Ryan amesema kuwa SAP ikishirikiana na taasisi mbalimbali
wamemekusudia kwa dhati kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya mia tano kutoka
Tanzania na zaidi ya walimu elfu tano kutoka Afrika wakiwa na lengo la
kuwafikia wanafunzi na watoto zaidi ya milioni moja na nusu Afrika nzima.
Kwa upande
wake Afisa Miradi wa taasisi ya Apps and Girls, Jesca Mmari amesema kuwa
wanakusudia kuwafundisha walimu programu iitwayo scratch ambayo itatoa hamasa na hamu ya wanafunzi kupenda kujifunza
teknolojia ambpo amewataka walimu walioko kwenye mafunzo hayo wapende na
wajitume kujifunza kuhusu programu hiyo na teknolojia kwa ujumla
ili waweze kuwafundisha wanafunzi kikamilifu.
Akizungumza mmoja wa walimu katika mafunzo hayo,Mussa Awadhi kutoka shule ya sekondari Benjaminj
Mkapa, amesema kuwa programu ya scratch inamuwezesha mwanafunzi kuelewa
kwa urahisi masuala ya teknolojia kwani imetengenezwa kwa mfumo wa picha
(katuni)na ni rahisi kujifunzia. imeanza kutoa mafunzo ya Programming kwa walimu kutoka

(katuni)na ni rahisi kujifunzia.
No comments:
Post a Comment