RC MAKONDA ATOA MWEZI MMOJA KWA TBA KUKAMILISHA UJENZI WA JENGO LA MANISPAA YA UBUNGO, AGOMA KUKABIDHI MRADI HUO KWA CCM - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, June 30, 2020

RC MAKONDA ATOA MWEZI MMOJA KWA TBA KUKAMILISHA UJENZI WA JENGO LA MANISPAA YA UBUNGO, AGOMA KUKABIDHI MRADI HUO KWA CCM


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wakazi wa jimbo la Kibamba wakakati akikabidhi mradi wa standi mpya ya kisasa ya mabasi inayojengwa mbezi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukabidhi miradi Mbalimbali iliyotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa Chama cha Mapinduzi CCM na kuwahimiza Wananchi kuchagua Viongozi wanaoweza kutatua kero zao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na wakazi wa jimbo la Kibamba wakakati akikabidhi mradi wa standi mpya ya kisasa ya mabasi inayojengwa mbezi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukabidhi miradi Mbalimbali iliyotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa Chama cha Mapinduzi CCM na kuwahimiza Wananchi kuchagua Viongozi wanaoweza kutatua kero zao.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori  akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kukabidhi miradi Mbalimbali iliyotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa Chama cha Mapinduzi CCM na kuwahimiza Wananchi kuchagua Viongozi wanaoweza kutatua kero zao.
Mkurugenzi wa Manspaa ya Ubungo Beatrice Dominic akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kukabidhi miradi Mbalimbali iliyotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa Chama cha Mapinduzi CCM na kuwahimiza Wananchi kuchagua Viongozi wanaoweza kutatua kero zao.
Mwenyekiti wa chama Wilaya ya Ubungo Ndg.Lucas Mgonja akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ya kukabidhi miradi Mbalimbali iliyotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa Chama cha Mapinduzi CCM na kuwahimiza Wananchi kuchagua Viongozi wanaoweza kutatua kero zao.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maulid Mtulia  mwenye tisheti ya njano katikati akipiga kwata pamoja na vijana wa hamasa wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipotembelea na kukabidhi kituo cha afya kilichopo Kimara mwisho
Mkuu wa Mkoa akipiga kwata na vijana wa hamasa Picha zote na Brian Peter

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amegoma kukabidhi kwa Chama cha Mapinduzi CCM Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Manispaa ya Ubungo kutokana na ujenzi huo kusuasua hadi sasa ambapo amemtaka Mkandarasi wa ujenzi huo Wakala wa Ujenzi TBA kuhakikisha anakabidhi mradi ndani ya mwezi mmoja kuanzia Leo.

RC Makonda amechukizwa kuona ujenzi huo ulitakiwa kukamilika na kukabidhiwa Mwezi Disemba mwaka jana lakini mkandarasi aliomba kuongezewa miezi sita lakini hadi sasa Ujenzi haujakamilika jambo lonaloendelea kuwafanya Watumishi wa Manispaa hiyo kufanya kazi katika mazingira magumu.

Hayo yamejiri wakati wa Mwendelezo wa Ziara ya RC Makonda kukabidhi miradi kwa Chama Cha Mapinduzi CCM ambapo kwa siku ya leo amekabidhi miradi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 196.4 kwa upande wa Jimbo la Kibamba.

Miongoni mwa miradi aliyokabidhi RC Makonda ni Stand ya Mabasi ya Mikoani ya Mbezi Luis inayogharimu Bilioni 50, Upanuzi wa Barabara ya Kimara hadi Kibaha yenye urefu wa Km 19.2 na gharama ya Bilioni 140.4, Upanuzi wa Mtambo wa Maji Ruvu Juu na ujenzi wa Tank Kibamba wa thamani ya Milioni 624.

Aidha RC Makonda pia amekabidhi mradi wa Ujenzi wa Mabanda Saba ya Wafanyabiashara Mbezi Luis unaogharimu Bilioni 1.5 na Ujenzi wa Kituo cha Afya Kimara Bilioni 1.5.

Ziara ya RC Makonda itaendelea siku ya kesho kwenye Jimbo la Ubungo ambapo atakabidhi miradi mbalimbali ya Maendeleo.

 HABARI KATIKA PICHA






















No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages