Arif Jinnah na mwanawe Amour Arif mwenye umri wa miaka 21 ni marubani shupavu katika Kampuni ya Shirika la ndege la Air Tanzania!
Jinnah anafahamika kwa kuendesha ndege ya Airbus A220 ilhali mwanawe ambaye ni msaidizi (Afisa wa kwanza) wake anarusha ndege aina ya Bombardier Q400. Amour ameripotiwa kuwa ndiye rubani mwenye umri mdogo sana katika shirika la safari za ndege nchini Tanzania.
Kwa mtazamo wa picha, wawili hao wanafanana kama shilingi kwa ya pili na ni rahisi sana mtu kukosa kuwatofautisha.
Capt. Arif Jinnah amekuwa rubani kwa zaidi ya miaka 33 na ametajwa kuwa bora zaidi nchini humo.
No comments:
Post a Comment