AIRTEL NA PRECISIONAIR WASHUSHA BEI TIKETI KWA WANAOLIPIA KUPITIA AIRTEL MONEY - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Friday, November 5, 2021

demo-image

AIRTEL NA PRECISIONAIR WASHUSHA BEI TIKETI KWA WANAOLIPIA KUPITIA AIRTEL MONEY

Kampuni ya simu za mkononi Airtel imeingia ubia na na kampuni inayotoa huduma za usafiri wa anga nchni PrecisionAir kwa kuzindua promosheni mpya itakayowawezesha wateja wake nchini kufurahia punguzo la asilimia tano kwa wateja wote watakaolipia tiketi za kusafiri na PrecisionAir kupitia Airtel Money.

Airtel Money na PrecisionAir wametangaza kuanza kwa promosheni hiyo maalum leo ambapo utawapatia wateja wa Precision Air urahisi katika kupanga safari zao na kuwawezesha kununua ticket zao wakati wowote kupitia huduma ya Airtel Money.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Airtem Money Bw, Isack Nchunda alisema "ushirikiano wetu tunaotangaza leo utawaongezea wateja wetu wa Airtel urahisi na uhakika wakati wa kulipia safari zao za ndani na za nje kwa kufanya malipo kidigitali pale wanapohitaji tiketi wakiwa popote .

kupitia ofa hii mpya sasa wateja wetu wataweza kufanya malipo ya tiketi zao za ndege kupitia huduma ya Airtel Money kisha mteja atapata punguzo la asilimia tano ya pesa aliyolipia tiketi hiyo. “ujio wa makubaliano haya unadhihirisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora za malipo kidigitali huku tukiwahakikishia wateja unafuu zaidi kwa kuwarejeshea kiasi cha pesa hizo ili wazitumie kufanya mambo yao mengine”. Aliongeza Nchunda

Akiongelea kuhusu ushirikiano huo Mkuu wa Biashara wa Precision Air Bi Lilian Mremi alisema “ushirikiano huu umekuwa wakati muafaka ambapo Precision Air ikiwa imejipanga zaidi kuwahudumia wateja kwa nakufanya huduma za usafiri wa anga kuwa zakipekee

Wateja wetu sasa wanaweza kufanya malipo ya tiketi zao za ndege kupitia huduma ya Airtel Money. Hii maana yake ni kujihudumia mwenyewe kupitia simu yako ya mkononi, mteja unaweza kutembelea tovuti yetu XXXXX kufanya booking ya safari kisha akalipia kupitia Airtel Money na kupokea tiketi yake ya kielectroniki kupitia simu yake ya mkononi” aliongeza Mremi

Akiongea kuhusu namna ya kupata huduma hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” huduma hii ni rahisi kutumia , mteja anachotakiwa kufanya ni kufanya booking ya safari au kufanya booking kupitia tovuti ya Precision Air ambapo mteja atapewa namba ambayo itatumika kama kumbukumbu/ reference wakati wa malipo. Kununua tiketi kupitia Airtel Money wateja wanatakiwa kufanya yafuatayo Piga *150*60#
  • Chagua namba 5 (Lipia bili)
  • Chagua namba 2 (Chagua kampuni)
  • Chagua namba 3 (Usafiri wa anga)
  • Chagua namba 2 (PrecisionAir)
  • Ingiza Kiasi cha pesa
Ingiza namba ya Kumbukumbu-(booking number)

Vilevile ipo njia nyingine mteja anaweza kuitumia kwa kuingia kwenye My AirtelApp na kufuata utaratibu huo. Mara baada ya mteja kufanya hayo atapokea ujumbe wenye uthibitisho wa malipo na tiketi yake “aliongeza Mmbando.

Jinsi ya kununua tiketi yenye punguzo

• Tembelea tovuto ya PresisionAir

• Chagua ndege na tarehe ya safari yako

• Chugua namba ya siti

• Ingiza namba yako ya offa/ ATLPW

• Pata kiasi kamili cha punguzo

• Lipa kupitia Airtel Money
.com/img/a/
Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda (kushoto) na Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Lillian Masawe wakionyesha bango baada ya kutangaza ushirikiano mpya ambapo kuanzia sasa wateja wa Airtel watakuwa wanapata punguzo la hadi asilimia 5 pale wanapolipia tiketi kwa kupitia huduma wa Airtel Money.
.com/img/a/
Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza ushirikiano baina ya Airtel Tanzania na Precision Air ambapo kwa sasa wateja watapata punguzo la hadi asilimia tano wanapolipia tiketi kwa kupitia Airtel Money. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara Precision Air Lillian Masawe.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *