BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO (TADB) YAAHIDI KUENDELEA KUINUA ZAO LA ZABIBU NCHINI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Saturday, November 6, 2021

demo-image

BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO (TADB) YAAHIDI KUENDELEA KUINUA ZAO LA ZABIBU NCHINI

6cf07022-16f2-4fb1-b0e9-af342f5a51cb 7f675d57-eda6-4288-8c77-426d29d35bfa 9e985219-9069-479a-9765-fd3ff119268e 793f813b-4e0d-41fd-9525-f77633fa72b9 f06ece9a-68f1-40c6-8c11-57c465af8bc5

Na.Alex Sonna, Dodoma | Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) imeahidi kuendelea kuinua zao la zabibu nchini ili kuwezesha kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki hiyo, Yodas Mwanakatwe wakati wa Tamasha la Mvinyo Dodoma maarufu kama Dodoma Wine Festivals.

Meneja huyo amesema kuwa TADB imewezesha wazalishaji wa zao la zabibu pamoja na wachakataji wa zao hilo.

Tumeweza kutoa mikopo yenye zaidi ya thamani ya Tsh. Mil 700 na kunufaisha watu 186 waliopo katika mnyororo wa thamani wa zao la zabibu.” amesema Mwanakatwe

Kwa mipango ya mbeleni, Mwanakatwe ameeleza kuwa benki hiyo inajipanga pia ili kuweza kuwawezesha wakulima zaidi na waongezaji thamani wa zao la zabibu wakati na wakubwa ili kukabiliana na tatizo la upotevu wa zabibu baada ya kuvunwa.

Kwa upande wake mmoja wa wanufaika wa mikopo hiyo, Katibu wa Chama cha Ushirika Wakulima wa Zabibu na Masoko Mpunguzi (WAMAZAMA), Emmanuel Temba ameishukuru benki hiyo kwa mkopo uliowawezesha kuanza kuzalisha mvinyo.

Awali tulipata changamoto ya kuweza kununua na kulipa kwa wakati wakulima wetu. Baada ya mkopo kutoka TADB, sasa tunalipa kwa wakati na wakulima wamepata uhakika wa soko la mazao yao wanapovuna."

Baada ya mkopo wa TADB, WAMAZAMA pia wameweza kununua mashine zinazotumika kuongeza thamani zao la zabibu kwa kutengeneza na kuhifadhi mchuzi wa zabibu (grape concentrate).

Mchuzi huu wa zabibu tunawauzia wazalishaji wa mvinyo wakubwa. Hii imetusaidia kuongeza tija kwenye kilimo cha zabibu. Wakulima wetu sasa wanapata kipato zaidi,” ameeleza Katibu huyo.

Tanzania inauwezo wa kuzalisha tani 150,000 ya zabibu na kwa sasa inazalisha wastani wa tani 16,000 tu. Hii inatoa fursa kwa vijana na wadau wengine kuwekeza katika sekta hii.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *