Wednesday, March 23, 2022

TANZANIA YAFAFANUA MSIMAMO WAKE KUHUSU MGOGORO WA URUSI NA UKRAINE
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mahojiano na moja ya vyombo vya Habari vya China. Mahojiano hayo yalifanyika kwa njia ya mtandao Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari kutoka China.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam | JAMHURI ya Muungano wa Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu sababu ya kupiga kura ya kutofungamana na upande wowote katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mgogoro unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine huku ikisisitiza pande zote mbili kutafuta suluhu katika meza ya mazungumzo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametoa ufafanuzi huo wakati akifanya mahojiano na mojawapo ya vyombo vya Habari kutoka China na kuongeza kuwa Sera ya Tanzania kuhusu namna ya kutatua changamoto za migogoro inapojitokeza ni kwa kutumia njia za kidiplomasia.
Balozi Mulamula amesisitiza kuwa Sera ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijabadilika tangu uhuru na kuongeza kuwa Tanzania inaamini hakuna mgogoro ambao hauwezi kutatulika hasa panapokuwepo na utashi na nia njema ya kumaliza mgogoro na kwamba njia ya kidiplomasia ndio chaguo sahihi kwa Tanzania kuhusu namna bora ya kumaliza mgogoro kati ya Urusi na Ukraine.
“Sisi msimamo wetu na Sera yetu na msingi wetu wa Sera yetu ya Mambo ya Nje ni kutofungamana na pande zozote, hivyo kutokupiga kura ni kuonesha msimamo wa Tanzania,” amesema Balozi Mulamula
Alipoulizwa endapo Tanzania imeathirika na vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine, Balozi Mulamula amesema madhara yanayotokana na vita hiyo yanajionesha dhahiri huku akitaja baadhi ya madhara hayo kwa baadhi ya wanafunzi wa kitanzania waliokuwa wanasoma nchini Urusi kukatisha masomo yao na kurejea nchini wakisubiria vita kumalizika pamoja na ongezeko la bei ya petroli na gesi duniani.
Kutokana na vita inayoendelea kati ya Ukraine na Urusi Tanzania ililazimika kuwaondoa raia wake nchini Ukraine hususan wanafunzi takribani 300 waliokuwa wakisomea masuala ya udaktari nchini humo.
Tags
# KIMATAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
BASATA YAMPIGA STOP STEVE NYERERE
Older Article
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA EQUITY KATIKA KILELE CHA WIKI YA MAJI
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi
Hassani MakeroFeb 16, 2025RAIS SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA MSUMBIJI
Hassani MakeroFeb 15, 2025A Tanzania doctor receives International Award
kilole mzeeJan 15, 2025
Labels:
KIMATAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment