UCHEBE WA SIMBA ATUA IHEFU FC - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, June 7, 2024

UCHEBE WA SIMBA ATUA IHEFU FC

Klabu ya Ihefu FC ambayo Msimu Ujao 2024-2025 Itajulikana kama Singida Black Stars Imetangaza yakuwa Imeingia Makubaliano na aliyewahi kuwa Kocha wa Simba 𝐏𝐚𝐭𝐫𝐢𝐜𝐤 𝐀𝐮𝐬𝐬𝐞𝐦𝐬.

Patrick Aussems Mbelgiji huyu anakumbukwa na Wanasimba kwa Kuwaongezea Kombe Msimu wa 2018-2019.

Ihefu wamempa Kandarasi ya Mwaka Mmoja kwa Maana Mkataba wake Utaisha Juni 30, 2025 Ukiwa na Kipengele cha Kuongeza Mwaka Mmoja na Kuendelea.

Pia amefundisha timu za taifa mbalimbali zikiwemo za Nepal na Benin. Kocha Aussems amewahi pia kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Marbella FC ya Uhispania.

Patrick Aussems Rasmi ataanza Kazi Mwezi Julai 1,2024 akiwa na Miamba hiyo ya Kutokea Mbarali Mbeya na sasa Ipo Singida Mkoani Singida. Kwasasa anaendelea na zoezi la usajili kwa kushirikiana na menejimenti.

Vilabu alivyowahi Kufundisha Uchebe.

Kafundisha Klabu (17) Tangu Mwaka 1992 Mpaka Mwaka 2021.

2013-14 ___ AC Leopard
2015-16 ___ Al Hilal
2016-17 ___ Nepal FC
2018-19 ___ Simba SC
2019-20 ___ Black Leopards

Kwa Ufupi Mwamba analijua soka la Kiafrika Kazi kwao IHEFU.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages