CHIFU WA WANGONI ALIVYOZIKWA NA WATU WAWILI WAKIWA HAI SONGEA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, June 23, 2024

CHIFU WA WANGONI ALIVYOZIKWA NA WATU WAWILI WAKIWA HAI SONGEA

Kaburi la mviringo alilozikwa Chifu Mharule Zulu Gama wa Songea na watu wawili wakiwa hai mwaka 1889.
Mzee Christian Ngonyani anayesimamia Mila na desturi katika kijiji cha Mbingamharule wilayani Songea.

Na Albano Midelo, Songea

MOJA ya vivutio vya utalii wa kiutamaduni vinavyopatikana katika kijiji cha Mbingamharule wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ni uwepo wa kaburi la duara ambalo Chifu Nkosi Mharule bin Zulu Gama alizikwa mwaka 1889.

Mambo ambayo yanawashangaza wengi wanaotembelea kaburi hili ni historia inayoonesha kuwa Nkosi Mharule baada ya kufariki alizikwa kwa desturi na mila za kichifu za kabila la wangoni toka Afrika ya kusini.

Christian Ngonyani mwenye umri wa miaka 90 ni mzee wa Mila katika kijiji cha Mbingamharule anasema kijiji hicho kimepewa jina la Chifu huyo ambaye alitokea nchini Afrika ya kusini na kutawala ungoni kuanzia mwaka 1847 hadi 1889 alipofariki na kuzikwa katika kijiji hicho.

Chifu Mharule baada ya kufa mwaka 1889 alizikwa kwa taratibu za jadi ya machifu wa Afrika ya kusini, kaburi lake lilikuwa la mviringo, sanda yake ilikuwa ya ngozi, alikalishwa kwenye kiti cha ngozi, walikamatwa watu wawili wakiwa hai walizikwa naye wakiwa wamesimama mbele na nyuma ya chifu, alisimulia mzee Ngonyani.

Amezitaja taratibu za kijadi za wakati huo zilitaka Mfalme au Chifu anapofariki ni lazima azikwe na watu wawili wakiwa hai na kusisitiza kuwa hiyo ilikuwa ni amri ya serikali ya jadi na hapakuwepo mtu aliyepinga.

Hata hivyo Mzee Ngonyani amewataja waliokuwa wanazikwa wakiwa hai na Mfalme ni wale ambao walikuwa wamezoeana na kufanyakazi naye kwa karibu.

Amesema kaburi hilo linatumiwa na wananchi wa kijiji hicho kwenda kuhiji kila mwaka kwenye kaburi hilo ambalo lipo kilometa mbili toka kijijini hapo na kwamba ndugu wa Chifu Mharule toka Afrika ya Kusini huwa wanafika kufanya matambiko kwenye kaburi hilo.

Amesema ukoo wa Mharule toka Afrika ya kusini walifika kushuhudia kusimikwa kwa Chifu Nkosi Imanuel Zulu Gama wa Tano ambaye ndiyo chifu wa wangoni wa sasa.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages