ZHSF Yakutana na Uongozi wa Hospitali za Serikali Kuimarisha Utoaji Huduma za Afya - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, June 6, 2024

ZHSF Yakutana na Uongozi wa Hospitali za Serikali Kuimarisha Utoaji Huduma za Afya

Afisa uthibitishaji watoa huduma Mfuko wa huduma za afya (ZHSF) Bakar Mbarak Anas akiwasilisha mada katika kikao cha kujadili changamoto za utoaji wa huduma kwa hospitali za umma kupitia mfuko huo huko Ukumbi wa ZSSF Kariakoo Wilaya ya Mjini.

Na Takdir Ali. Maelezo Zanzibar.

Madakari wa Hospitali za Serikali wametakiwa kuongeza bidii ya kufanya kazi ili kukabiliana na ushindani wa hospitali binafsi katika kutoa huduma.

Hayo yameelezwa na Afisa Uthibitishaji watoa huduma kutoka Mfuko wa huduma za Afya (ZHSF) Bakari Mbarak Anas alipokuwa akifunguwa kikao cha Watoa huduma wa Hospitali za Serikali na vituo vya Afya vilivyo chini ya Jeshi la Polisi huko katika Ukumbi wa ZSSF Kariakoo Wilaya ya Mjini.

Amesema Serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo kujenga hospitali na kuajiri madakatari lakini bado muitikio wa wagonjwa wanaotumia ZHSF kuenda Hospitali hizo ni mdogo, ikilinganishwa na Hospitali binafsi.

Aidha amewataka watoa huduma hao, kuwa na mapokezi mazuri na kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu ili kuongeza idadi ya Wagonjwa wanaokwenda kupata matizbabu katika hizo.

Mbali na hayo amesema azma ya Serikali kuanzisha ZHSF ni kuwasaidia wananchi kupata huduma bora za afya hivyo juhudi za pamoja zinahitajika katika kufikia malengo hayo.

Nao washiriki wa kikao hicho akiwemo Salma Ubwa kuto hospitali ya wilaya ya magharibi A Mbuzini na Hamdani Pande Hamdani kutoka kituo cha Afya Polisi Ziwani wameomba kuongezewa Madakati waliobobea katika maradhi mbalimbali (specialist) ili kuweza kuwashawishi Wanachama kutumia Hospitali hizo.

Aidha wameishauri Serikali kutenga eneo maalum la wateja wa Mfuko ili kuondokana na mrundikano wa wagonjwa jambo ambalo amelitaja kusababisha baadhi ya wagojwa kukimbilia hospitali binafsi.

Katika kuhakikisha ZHSF inafikia lengo la Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi waote, wameweka utaratibu wa kukutana na watoa huduma wa hospitali za Serikali na binafsi ili baini changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi unaofaa.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages