Tuesday, March 21, 2017

SHISTAMA wajipanga kujisalimisha BASATA
SHIRIKISHO
la Sanaa za Maonesho Tanzania (SHISTAMA) linajipanga kupeleka mpango kazi wake
kwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kabla ya uzinduzi wa Shirikisho hilo.
Akizungumza
na Wor’Out
Media jana, Rais wa Shistama, William Chitanda ‘MC Chitanda’ baada
ya mipangilio kutoka BASATA, watatengeneza Kalenda itakayokuwa na mgawanyo wa
majukumu ya Shirikisho hilo.
MC
Chitanda alisema mikakati mingine watakayoitekeleza ni kuwatambua na kuongeza
idadi ya wanachama wenye usajili unaotambulika na Shirikisho hilo.
“Tunatambua
baadhi ya wasanii wengine hawajajiunga katika vyama ili Shirikisho liwe na
nguvu ambayo itasongesha mbele maendeleo ya Shirikisho”, alisema MC Chitanda.
MC
Chitanda alisema mikakati yao itafanikisha kukuza na kuendeleza uchumi ambako
pia wanajipanga kuunda miradi kama SACCOS na Benki ya Wasanii.
Tags
# MICHEZO
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
‘YAH TMK’ yarekodi mbili kali ‘kideoni’
Older Article
RUGE ATHIBITISHA MAKONDA KUIVAMIA CLOUDS MEDIA AKIWA NA SILAHA
Milioni Mbili za Mbunge Ummy Mwalimu zilivyochochea ushindi wa Coastal Union
Hassani MakeroApr 14, 2025RAIS SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MMILIKI WA KLABU YA MANCHESTER UNITED YA UINGEREZA IKULU JIJINI DAR LEO
Hassani MakeroApr 11, 2025NBC Kutumia Mchezo wa Gofu Kuchochea Ushirikiano wa Kibiashara
Hassani MakeroMar 24, 2025
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment