Wavuvi
katika bwawa la Mabayani Pande Mkoani Tanga wakimuonyesha samaki aina ya Mkunga
waliemvua jana, Samaki huyo walimuuza kwa shilingi 10,000.
Bwawa
la Mabayani ndio linalotegemewa kwa matumizi ya maji Tanga ambapo kwa sasa watu
wanaoshukiwa kuwa wachimbaji wa madini kwenye vyanzo vya maji katika milima ya
Amani Wilayani Muheza wamekuwa wakiyachafua hali ambayo Mamlaka ya maji safi na
Maji taka ikipambana na kuhakikisha maji hayo hayachafuliwi.
Hata
hivyo kwa uharibifu huo Mamlaka ya Maji safi na Majitaka imekuwa
ikigharamika kuhakikisha maji hayo licha ya kubadilika rangi hayana madhara
kwa mtumiaji.
Tanga
Uwasa imekuwa ikifanya ziara mara kwa mara katika vyanzo vya maji katika Milima
ya Amani na kuwataka wachimbaji madini kuacha kuchimba kwa madai kuwa kipindi
hiki cha mvua bwawa lake hupokea maji yenye rangi ya tope tope.
No comments:
Post a Comment