Wednesday, June 28, 2017

“Mtamkumbuka na Mtalia” Lampard awaambia Chelsea kuhusu Costa
Tayari kocha Antonio Conte amemuambia
Diego Costa atafute pakucheza msimu ujao, hilo linakuja baada ya mshambuliaji
huyo kutoa mchango mkubwa sana kwa klabu ya Chelsea na kuifanya kuchukua
ubingwa EPL.
Sasa kiungo wa zamani wa Chelsea Frank
Lampard amewaonya Chelsea kuhusu Costa na kusisitiza kwamba itawachukua muda na
itakuwa ngumu sana kwao kumtafuta Diego Costa mwingine.
Lampard anaona duniani kwa sasa kuna
uhaba wa washambuliaji aina ya Diego Costa na timu nyingi zinatamani kuwa na
mchezaji wa namna yake, hivyo Chelsea itawagharimu sana kumuacha aondoke.
“Hata sielewi, haihitaji kuongea sana
kuhusu yeye kwani kila kitu kinaonekana wazi, tangu amekuja Chelsea amekuwa
akionesha kiwango cha hali ya juu sana na nina mashaka makubwa kama wataweza
kuziba pengo lake” alisema Lampard.
Tangu ajiunge na klabu ya Chelsea
mwaka 2014 mshambuliaji huyo wakimataifa toka nchini Hispania amekuwa akiongoza
kwa ufungaji katika klabu hiyo kwa misimu mitatu mfululizo na akiwasaidia
kubeba makombe.
Lampard anasema Lukaku kweli ni mzuri
sana lakini ununuzi wake ni ghali na anaona ni bora wabaki na Costa ambaye ana
kila kitu ambacho mshambuliaji yoyote duniani anapaswa kuwa nacho.
Tags
# MICHEZO
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Barclays Bank Tanzania rewards its customers for switching to digital
Older Article
RayVanny afanya colabo na staa wa muziki Marekani Jason Derulo
TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI KUU TANZANIA
Hassani MakeroMar 08, 2025WAKAZI WA DAR WAJITOKEZA KUCHUKUA NAMBA KUSHIRIKI MBIO ZA YAS KILI INTANATION HALF MARATHON
kilole mzeeFeb 15, 2025KOCHA WA YANGA APEWA MKONO WA KWAHERI
Hassani MakeroFeb 04, 2025
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment