TAASISI YA AL-NOOR CHARTABLE AGENCY YAWAJENGEA MSIKITI WAKAZI WA CHANIKA DSM - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, January 28, 2018

TAASISI YA AL-NOOR CHARTABLE AGENCY YAWAJENGEA MSIKITI WAKAZI WA CHANIKA DSM




 Picha ya ramani ikionyesha namna msikiti   wa Al-rahma  utakavyo kuwa baada ya kukamilika.


Taasisi ya  AL-NOOR  CHARTABLE  AGENCY, leo imesaini  makubaliano ya Ujenzi wa Msikiti  mkubwa utakao jengwa katika  eneo la Zingiziwa Chanika jijini  Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo  iliyo fanyika katika  msikiti wa  Mahmuor  Upanga jijini Dar es Salaam, Shekh. Nasr  Tahdhanmy, amesema, ujenzi huo utaanza   kesho na utakamilika ndani ya miezi mitatu na utajulikana kwa jina la Masjid  Al -rahma,   utakuwa na uwezo wa kuswali watu 500 ndani  na nje.

Amesema,wameamua kujenga msikiti huo katika eneo hilo kwa kuwa kuna  Waislamu wengi na hawana Msikiti  hivyo watuwengi watapata  pahala pazuri pa kuabudu  kuliko hivi sasa ambapo wanapatashida .

Msikiti huo utakuwa mkubwa , utakuwa   na Maduka ,Clinic, sehemu ya kuoshea Maiti   , nyumba ya mayatima  Pamoja na nyumba ya Imamu.

‘’Nashukuru sehemu hii nikubwa  Masha- allha  na inawaislamu  wengi kama tulivyo ambiwa, na msikiti kuja kuujenga  huku mbali niliona siyo fikra nzuri  lakini nilipo kuja kushauriana na wenzangu  nikaona nifikra nzuri  tumeuchukua msikiti kuwa fuata  Waislam kuliko Waislamu  kuufuata msikiti, alisema.


Naye  Mkurugenzi  mkuu wa  taasisi hiyo Nadir Mahfoudh amesema kujenga msikiti kuwa fuata Waislamu nijambo zuri kuliko  kuendelea tu kujenga  misikiti maeneo ambayao  yako karibu na  barabara kuu, na sehemu hiyo ameona inafaa sana na kwamba malipo yatafanyika ili ujenzi huo uweze kuanza mara moja.

 Shek Nasr  Tahdhanmy wakwanza kulia,  akishudia  utiaji saini wa kujenzi  wa msikiti eneo la Chanika Zingiziwa yaliyofanyika Upanga jijini Dar es salaam. 
Picha ya ramani ikionyesha namna msikiti   wa Al-rahma  utakavyo kuwa baada ya kukamilika.
 Baadhi ya washiriki wa hafla ya utiaji saini ujenzi wa msikiti wakionesha  Picha ya 
ramani ikionyesha namna msikiti   wa Al-rahma  utakavyo kuwa baada ya kukamilika.



 Picha mbalimbali zikionyesha sehemu ambayo utajengwa Msikiti huo


No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages