Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mh.Paul Makonda akizungumza na wananchi hao leo jijini hapo.
Baadhi ya wananchi waliofika katika zoezi la kuwasilisha malalamiko yao ya kudhulumiwa mali zao.
Mmoja wa Mjane aliedhulumiwa akiwasilisha malalamiko kwa kilio.
Zaidi ya wananchi 3000,wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamejitokeza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Leo kuweza kuwasilisha mamalamiko yao ya kudhulumiwa Mali zao zikiwemo Nyumba,viwanja, Mirathi kwa lengo la kupata haki zao za msingi.
zoezi hilo limeanza Leo ambapo litadumu Kwa siku tano mfululizo ikiwa ni agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda la kuwataka wananchi wote wakazi wa Mkoa huo waliodhulumiwa Mali zao, kufika katika ofisi za Mkoa kuwasilisha malalamiko yao chini ya wanasheria wabobezi.
Akizungumza na wakazi hao waliofika kusikilizwa malalamiko yao, Rc Makonda amesema wananchi wote waliofika lazima watasikilizwa na wanasheria zaidi ya 160 waliojitoea kusikiliza wananchi hao wanaiteseka na kunyanyasika bila sababu ya msingi.
"Wananchi wametaabika Sana hivyo nimeona nivyema kuaandaa siku maalumu kwa ajiliyl yaykuwasikiliza chini ya wanasheria wangu waliojitokeza zaidi ya 160 kuweza kuwasikiliza na kuweza kupata haki zenu za msingi.
Amesema kutokana na wingi huo wa wakazi walioonewa inaonyesha dhahiri kuwa baadhi ya watu hawatendi kazi zao ipasavyo,hivyo watakaobainika watachukuliwa hatua.
"Umati huu wa wananchi wanyonge inaonyesha wapo wafanyakazi wa Serikali hawatendi kazi zao ipasavyo hivyo zoezi hili likiisha nitashughulika na wakuu wa idara zote ambazo hazikufanya kazi yake ipasavyo "Amesema Makonda.
Aidha amesema wananchi wote waliofika watasikilizwa kikamilifu na wanasheria hao waliobobea na baada watowasisha ili kujua nini kifanyike na kila mmoja aweze kupata haki zao kikamilifu.
Pia amewataka wanasheria kusikiliza kila mmoja anaefika kuwasilisha malalamiko hayo kuwasikiliza kwa makini kwa nzia mwanzo hadi mwisho na kuwasihi wasitoe hukumu wao
Kwa upande wa wananchi hao wamemshukuru Rc Makonda kwani ameweza kuwasidia,kuondokana na mateso ikiwa kunyanyaswa kwa zaidi ya miaka ishirini bila ya mafanikio.
Kwa Upande wake Fatuma Muhammad amesema amedhulumiwa kiwanja chake, na kuteseka kwa zaidi ya miaka kumi bila ya mafanikio hivyo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, wanamatumaini ya kupata haki zao za msingi.
No comments:
Post a Comment