Ndiyo hivyo, Simba imeshinda ndani na nje ya uwanja. Goli pekee la Erasto Nyoni kwenye pambano la Kariakoo Derby limeipa Simba pointi tatu na kuendelea kuusogelea ubingwa wa VPL msimu huu.
Ukiachana na ushindi huo, ushindi mwingine Simba wameupata nje ya uwanja ambapo wafanya biashara wa jezi wamethibisha kwamba katika mchezo huo wameuza jezi nyingi za Simba kuliko Yanga.
Wor'Out Media imefanya mahojiano na baadhi ya wauzaji wa jezi ambao wamekiri kupata kitita cha maana kutokana a mauzo ya jezi za Simba huku Okwi, Kichuya, Kwasi na Mkude wakiongoza kwa mauzo.
Hata uwanjani mashabiki wa Simba walionekana ni wengi ukilinganisha na watani zao kwa mujibu wa ukaaji. Upande ambao hukaa mashabiki wa Simba ulipendezeshwa na rangi nyekundu na nyeupe wakati upande wa Yanga kuna viti vingi vilikuwa havina watu.
No comments:
Post a Comment