Baada ya Yanga kupoteza mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba, mashabiki wa Yanga waliwazonga viongozi wa klabu hiyo wakilalamika kwamba hawataki kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa aendelee kuwepo kwenye benchi la ufundi.
Mashabiki walikuwa wanalalamikia mabadiliko yaliyofanywa na benchi la ufundi kwa kumtoa Papy Tshishimbi na nafasi yake kuchukuliwa na Emanuel Martin. Mabadiliko mengine yanayolalamikiwa ni kumtoa Ibrahim Ajibu na kumuingiza Pius Buswita.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Nsajigwa amesema Tshishimbi alipumzishwa kwa sababu aliumia na alikuwa akicheza huku anamaumivu.
No comments:
Post a Comment