Serengeti Boys yabeba ndoo Birundi - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, April 30, 2018

Serengeti Boys yabeba ndoo Birundi


Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys imetwaa ubingwa wa CECAFA U17 Championship nchini Burundi baada ya kuwafunga Somalia 2-0 katika mchezo wa fainali.
Mashindano hayo ni mwendelezo wa maandalizi kuelekea fainali za Afrika wa vijana wa umri huo ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo.
Baada ya mchezo kumalizika kocha wa timu hiyo Oscar Milambo amezungumzia mashindano kwa ujumla na nini ambacho wamekipata kama timu kuelekea fainali za mwakani.
“Tunashukuru kwa sababu tumepata kile ambacho tulikuwa tunakihitaji, lengo letu kuu ilikuwa ni kuoata uzoefu wa kimataifa na tulikuwa tumejiwekea kwamba mpaka tunarudi nyumbani angalau tucheze mechi tano.”
“Imekuwa bahati mbaya kwenye hatua ya makundi ya makundi tulicheza mechi mbili halafu nusu fainali na baadae fainali. Kupata michezo minne si haba vijana wetu wamepata uzoefu wa kimataifa lakini tunafarijika zaidi kupata hiki ambacho tumepata.”
“Tunaamini tupo kwenye njia sahihi kama tutaendelea kufanya maandalizi na vijana kupata uzoefu wa kimataifa ni suala la muda kabla mwaka 2019 haujafika vijana watakuwa wanapeperusha kwa dhati bendera ya Tanzania.”

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages