DK TULIA ACHANGIWA FEDHA ZA KUCHUKULIA FOMU YA UBUNGE NA VIONGOZI WA KIMILA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, July 9, 2020

DK TULIA ACHANGIWA FEDHA ZA KUCHUKULIA FOMU YA UBUNGE NA VIONGOZI WA KIMILA





Umoja wa viongozi wa kimila (MACHIFU) pamoja na Wazee wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya leo wamefika nyumbani kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na kumpatia pesa taslim ambazo wamezichanga kwa umoja wao ili ziweze kumsaidia kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo ambalo anatarajia kugombea kwenye uchaguzi mkuu 2020 ambalo hadi sasa hajalitaja.

Tumekuja kwa ajili ya kumtakia kila la kheri katika kule anakokwenda kugombea, sisi kama wazazi tumemkubalia na tunamtakia mafanikio mema huko anakotaka kwenda

Tunafahamu kwamba ametia nia ya kugombea nafasi ya Ubunge, kikubwa kilichotusukuma kufanya hiki leo ni kutokana na jitihada kubwa alizozifanya na anazozifanya katika taifa letu kwenye maeneo mbalimbali”- Joel Mwakatumbula, Mkuu wa Machifu Rungwe

Kwa upande wake Dkt. Tulia amesema "Niwashukuru sana Wazazi wangu hawa kwa upendo mkubwa walionionesha pamoja na Baraka zao, ni wazi pengine ningeweza kupungukiwa hiyo pesa lakini wakaona mtoto wetu asijekuacha kuchukua fomu kwa kukosa hiyo pesa. Hakika wameianzisha safari ambayo na wao wameona ulazima wa kuwa sehemu ya safari hiyo” –Dkt. Tulia.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages