MARUFUKU KWA WATENDAJI KUWACHANGISHA WAGOMBEA KWA MADAI YA KUTAKA KUIMARISHA CHAMA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, July 8, 2020

MARUFUKU KWA WATENDAJI KUWACHANGISHA WAGOMBEA KWA MADAI YA KUTAKA KUIMARISHA CHAMA


Na Suhaila Pongwa na Wahida Juma, Zanzibar

Mwenyekiti wa sekretarieti ya mkoa Ndg  Abdallah Mwinyi Hassan amesema Ni marufuku kwa watendaji wa Ngazi ya wadi na wilaya kuwachangisha wagombea wanaokwenda kuchukuwa fomu ya kutaka kuwania nafasi ya udiwani, uwakilishi na ubunge kwa madai ya kutaka kuimarisha  chama.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wajumbe chama cha mapinduzi wa majimbo ya Magomeni, Jang’ombe, Kikwajuni  na jimbo la malindi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake yenye  lengo la kutoa mafunzo ya vikao vya uchujaji kwa  majimbo 9 ya mkoa wa mjini kichama huko katika ukumbi wa tawi la CCM Matarumbeta.

Ndugu Abdallah ambae pia ni katibu wa ccm Mkoa wa Mjini amesema utaratibu uliowekwa na chama wa uchukuaji wa fomu kwa ngazi ya udiwani ni shilingi 10,000 na nafasi ya ubunge na uwakilishi shilingi 100,000 hivyo si vyema kwa watendaji kuwachangisha wagombea hao kwani kufanya hivyo ni kwenda   kinyume na utaratibu uliwekwa na chama.

Aidha amesema kuna baadhi ya watendaji walikuwa wakichangisha pesa kwa madai ya kutaka kuimarisha chama jambo ambalo halipo ndani ya chama CCM.

Ndugu Abdallah amewataka viongozi wanaoshiriki katika vikao vya uchujaji kujifunza namna ya kuhifadhi siri za vikao ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza.

Sambamba na hayo amesema ili chama cha mapinduzi kiweze kushinda ni lazima kwa wanachama hao kuchagua viongozi walio shiba sifa zote za uongozi ili kukirahisishia chama hicho kushinda katika uchaguzi mkuu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages