NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWASHUKIA WAAJIRI WASIOWASILISHA MICHANGO NSSF, ATOA MAAGIZO MAZITO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, July 2, 2020

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AWASHUKIA WAAJIRI WASIOWASILISHA MICHANGO NSSF, ATOA MAAGIZO MAZITO


Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde leo ameanza utekelezaji wa agizo la kuwachukulia hatua za kisheria waajiri wote wasiowasilisha michango ya wafanyakazi katika mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF.

Naibu Waziri Mavunde alitoa agizo tarehe 9.06.2020 la kuwataka waajiri wote ambao hawajawasilisha michango ya wafanyakazi katika mfuko wa NSSF kufanya hivyo ndani ya wiki mbili vinginevyo hatua kali dhidi yao kuchukuliwa.


"Kumkata Mfanyakazi michango ya NSSF kwenye mshahara na kutokuwasilisha michango katika mfuko kwa kubadili matumizi ya fedha hizo ni tendo la uwizi kama ulivyo uwizi mwingine wowote.

Nimetoa maagizo kwa Wanasheria wa NSSF kujadiliana na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ya Umma kama makosa haya ya kukata fedha za wanachama na kuzitumia kwa malengo tofauti bila kuwasilisha kwenye mfuko husika haidondokei katika makosa ya Utakatishaji fedha"Alisema Mavunde.



Wakati huo huo Naibu Waziri Mavunde ameelekeza kukamatwa na kuhojiwa kwa wamiliki wa Kampuni ya D.B. Shapriya Co Ltd kutokana na kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi,na pia kumtaka Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Q Rent Tanzania Ltd ,kupitia mawasiliano ya simu,kufika saa 3:00 na nyaraka zote za malipo ya wafanyakazi katika ofisi ya Meneja wa NSSF na kutoa maelezo kwanini asichukuliwe hatua kwa kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages