TAHA KUWAFUNDISHA WAJASILIAMALI WAO NJIA BORA ZA USINDIKAJI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, July 9, 2020

TAHA KUWAFUNDISHA WAJASILIAMALI WAO NJIA BORA ZA USINDIKAJI



Dar es Salaam.


Wakulima wanaojishughulisha na  Mazao ya kilimo biashara ya Mbogamboga, Matunda na Viungo maarufu kama ‘Horticultural’ wameshauriwa kujiendeleza kwa kujifunza namna bora ya kuongeza thamani Mazao yao kwa njia ya usindikaji.

Akiongea katika ziara maalum ya mafunzo ya namna ya usindikaji na vifungashio vya bidhaa kwenye Maonyesho ya Biashara ya 44 Sabasaba kwenye Banda la TWCC, Mratibu wa Jinsia na Lishe wa Tasisi inayojishughulisha na Kilimo cha Mbogamboga,Matunda na Viungo Nchini (TAHA) Salome Stephen, amesema kuwa wakulima wa mazao hayo wanaweza kufanikiwa Zaidi katika swala zima la usindikaji wa Mazao yao.

Amesema kuwa Taasisi yao yenye Makao yake Makuu Jijini Arusha imeweza kuwapeleka Wanachama wao 20 kutoka Arusha, Pemba na Unguja kwa lengo la kuona na kujifunza kutoka kwa wajasiliamali wenzao walioko chini ya TWCC namna bora ya usindikaji wa Mazao na kutengeneza mtandao na mahusiano baina yao.

“tumekuja na Wajasiliamali 2o hapa, hawa ni wasindikaji ili  kujifunza masuala ya usindikaji kutoka kwa wenzao na kutumia Vifaa vipya vya kufanya ‘Packaging’ na kujionea bidhaa mpya na Mashine Mbalimbali za Usindikaji” alisema Salome.

Aidha amesema kuwa TAHA ina lengo la kuendeleza tasnia ya ‘Horticultural’ Nchini kwa kujishughulisha na Mnyororo wa Mazao ya Mbogamboga, Matunda na Viungo ambapo wanawawezesha kwa kuwapa mafunzo ya Kiteecknolojia na mbinu bora za Kilimo Biashara.

“Sisi kama TAHA licha ya Masuala ya Mnyororo wa Mazao pia tunawapa wakulima wetu mbinu bora za Kilimo biashara na Tekinolojia ya kisasa ambapo inawasaidia kuweza kulima kilimo cha faida” alisema Salome.

Taasisi ya TAHA yenye Makao yake Makuu Jijini Arusha ina wanachama Zaidi ya elfu 40 nchi nzima katika mikoa  23 ya Bara na Visiwani.  

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages