RC MJEMA ARIDHISHWA NA UJENZI VYUMBA VYA MADARASA KAHAMA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Tuesday, November 9, 2021

demo-image

RC MJEMA ARIDHISHWA NA UJENZI VYUMBA VYA MADARASA KAHAMA

WhatsApp+Image+2021-11-09+at+11.05.51+PM+%25281%2529

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ameendelea na ziara yake ya ukaguzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo, ambapo kwa sasa yupo wilayani Kahama akitembelea Halmashauri zote Tatu za wilaya hiyo ili kuona hutua ilipofikia jenzi hizo.

Mjema amendelea na ziara hiyo leo wilayani Kahama, mara baada ya kumaliza kutembelea Manispaa ya Shinyanga, wilaya ya Shinyanga, na Kishapu, kuona hatua za ujenzi wa vyumba vya madarasa, na kuonesha kufurahishwa na Kahama, ambapo majengo yake yapo kwenye hatua ya kuoandisha Maboma, ufungaji, Renta na upauaji.
WhatsApp+Image+2021-11-09+at+11.05.52+PM
Akizungumza mara baada ya kumaliza kufanya ziara ya ukaguzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Msalala, na Manispaa ya Kahama, amesema amefurahishwa na kazi ya ujenzi huo, ambapo utafanya wafikie malengo ya kukamilisha mapema kabla ya Decemba 15, huku akiahidiwa Majengo hayo atakabidhiwa Novemba sababu yatakuwa yameshakamilika kujengwa.

"Wilaya ya Kahama kasi yenu ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ni nzuri sana nimeipenda, na muendelee na kasi hiyo hiyo, na kukabidhi madarasa Novemba 20 hadi 28 kama mlivyo niahidi," alisema Mjema.

"Nataka katika mkoa wa Shinyanga tuwe wa kwanza kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa," aliongeza Mjema.
WhatsApp+Image+2021-11-09+at+11.05.51+PM
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, alisema katika wilaya hiyo wamepokea fedha za ujenzi wa vyumba vya Madarasa Sh.bilioni 5.5 ambapo wanajenga Madarasa 247, na yote yapo katika hatua nzuri za ukamilishaji.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *