Director Khalfani Afariki Hospitali Ya Muhimbili, Kuzikwa Leo Makaburi Ya Kisutu - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, May 5, 2024

Director Khalfani Afariki Hospitali Ya Muhimbili, Kuzikwa Leo Makaburi Ya Kisutu

Muongozaji wa video za muziki nchini Tanzania ‘Director Khalfani Khalmandro’ amefariki Dunia leo asubuhi Mai 5, 2024 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa zilieleza kuwa Khalfani alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, taasisi ya mifupa MOI akiwa na tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo lililopelekea changamoto ya kupooza upande wake wa kulia wa mwili.

Enzi za Uhai wake alijipatia umaarufu kwa kuongoza Video za Wasanii kama Aslay, NavyKenzo, Christian Bella, Baby Madaha, Chinbees, Shilole na Linah

Maziko yatafanyika saa kumi jioni katika makaburi ya Kisutu baada ya swala katika Msikiti wa Maamoor ambapo kwa sasa msiba upo upanga mwanzoni mwa mtaa wenye Diamond Jubilee (kama unatokea upande wa msikiti wa Wahindi)

Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wote wa sanaa ya Director Khalfani katika nyakati hizi ngumu!

Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages