Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zenj Flava Visiwani Zanzibar, Rico Single Afariki Dunia - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, June 7, 2024

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zenj Flava Visiwani Zanzibar, Rico Single Afariki Dunia

Msanii wa Muziki Rashid Amini Abdallah Maarufu kama Rico Single, amefariki Dunia Asubuhi ya kuamkia Leo Tarehe 7/06/2024,

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Dada yake aitwae Sofia anasema Msanii huyo alianza kuumwa juzi hali iliyompelekea kuharisha na kutapika ikabidi wampeleke hospitali, ambapo akapatiwa drip na kurudi nyumban jana akiwa na Afadhali.

Lakini kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, Alfajiri ya leo saa 12 akafariki akiwa nyumbani kwa dada yake huyo,

Maziko yamefanyika leo saa 10 jioni Msikiti wa Wales Kikwajuni, Wilaya ya Mjini Unguja na kuzikwa Makaburi ya Mwanakwerekwe visiwani Zanzibar.
M/mungu aipumzishe Roho ya marehemu mahala pema Peponi AMIN.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages