WAZAZI MKOA WA MAGHARIBI WAFANYA KONGAMANO KUELEKEA WIKI YA WAZAZI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, May 5, 2024

WAZAZI MKOA WA MAGHARIBI WAFANYA KONGAMANO KUELEKEA WIKI YA WAZAZI

Mkuu wa Oganaizesheni Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Omar Ibrahim Kilupi akifunguwa kongamano la jumuiya ya wazazi wa Mkoa wa Magharibi Kichama, lililofanyika skuli ya Ali Hassan Mwinyi Bububu Wilaya ya Magharibi A.

Na Fauzia Mussa, Zanzibar

Mkuu wa Oganaizesheni Afisi Kuu ya chama cha mapinduzi Zanzibar Omar Ibrahim Kilupi amezitaka jumuiya za chama cha Mapinduzi kuweka mikakati ya kuwatambua vijana ambao hawajasaliliwa katika datfari la wapiga kura ili waweze kusajiliwa.

Akifungua kongamano la jumuiya ya wazazi wa Mkoa wa Magharibi Kichama huko Skuli ya Ali Hassan Mwinyi Bububu amesema kuna baadhi ya vijana hawakujiandikisha katika awamu iliopita hivyo ni vyema kuwatambua na kuwahamasisha kujiandikisha katika awamu ijayo.

Amezitaja baadhi ya sababu zilizopelekea vijana hao kutojisajili kuwa ni pamoja na kutotimiza umri wa miaka 18 pamoja na kuwa mbali na vituo vya kujiandisha kwa kipindi hicho.

Aidha amezitaka jumuiya hizo, kuhakikisha vijana wote waliotimiza vigenzo wanajisajili ili kuweza kupata vijana wengi watakaoendelea kukiweka madarakani chama cha Mapinduzi ifikapo 2025.

Kuna kundi la wananchi ambao wana sifa za kujisajili lakini hawajaenda kujisajili na kama tunavyojuwa kama hukujisajili katika daftari la kudumu la wapiga kura hutoweza kupiga kura, tuendeni tukahamasishe ili tusije kumuacha mtu nyuma.” alisema Kilupi.

Aidha amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu ya uchaguzi na mmongonyoko wa maadili na kuwataka kuyafanyia kazi mafunzo walipopewa sambamba na kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao.

Kwa upande wake Mlezi wa Mkoa wa magharibi kichama ambae pia Mwakilishi wa viti maalum kupitia jumuiya ya wazazi mkoa wa kusini Unguja Mhe. Sabiha Filfil Thani amesema kuna kila sababu ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuendelea kubaki madarakani katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani kutokana na kutekeleza kwa vitendo ilani ya chama hicho.

Ilani ya CCM ilimtaka rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kujenga madarasa 1,500 kwa Skuli za Unguja na Pemba ambapo amevunja rikodi kwa kujenga madarasa 2273 sawa na silimia 150 ya malengo ya ilani ya chama cha Mapinduzi.” amefahamisha Mlezi huyo.

Katika kongamano hilo mada mbili ziliwasilishwa na kujadiliwa ikiwemo mmongonyoko wa maadili na Uchaguzi Mkuu ambapo Kauli mbiu ni "USHINDI WA CCM 2024-2025 JUMUIYA YA WAZAZI TUPO MSTARI WA MBELE”.
Mlezi wa Mkoa wa magharibi kichama ambae pia Mwakilishi wa viti maalum kupitia jumuiya ya wazazi mkoa wa kusini Unguja Mhe. Sabiha Filfil Thani akizungumza katika kongamano la jumuiya ya wazazi Mkoa wa Magharibi Kichama huko Skuli ya Ali Hassan Mwinyi Bububu Mkoa wa Mjini Magharibi.
Vijana wa Sanaa wa kikundi cha Toto boy Hawai Ibrahim Juma Shaaban na Hamad Seif Mohammed wakitoa burudani yenye maadhui ya athari za mmomonyoko wa maadili katika Kongamano la jumuiya ya wazazi, lililofanyika Skuli ya Ali Hassan Mwinyi Bububu Unguja.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages