OPERESHENI YA DOREEN YAFANIKIWA MAREKANI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Friday, May 19, 2017

demo-image

OPERESHENI YA DOREEN YAFANIKIWA MAREKANI

3

Habari kutoka Hospitali zinasema Mtoto Doreen amemaliza salama kufanyiwa upasuaji wa UTI wa MGONGO, kwa kile ambacho madaktari wamesema kumefanikiwa kwa ufanisi mkubwa kupita matarajio yao.

Mtoto Doreen alikuwa afanyiwe upasuaji kwa makadrio ya masaa 5:30, lakini zoezi hilo lilikamilika kwa muda wa masaa 4:00, huku TEAM ya "Surgical Support" ikiwa na watu 6, na kwa pamoja wakiongozwa na madaktari bingwa 2, Dr. Meyer na Dr. Durward. Doreen amehamishwa kutoka chumba cha upasuaji na kupelekewa ICU, na madaktari wamesema kwa kuwa hali yake imeridhisha sana, baadaye leo watamtoa ICU na kumrudisha wodi ya watoto ambako ataendelea na mapumziko.

MUNGU amesikia MAOMBI ya watanzania na wote waliotoa SALA na DUA zao kwa ajili ya mtoto Doreen popote Duniani.

1

Mtoto Wilson kwa mara kwanza ametoka nje ya Jengo Kuu la Hospital ya Mercy akiwa kwenye "wheelchair", huku Mama na Daktari wake wakiwa na tabasamu.
2


Mtoto Sadia akiwa na Dkt. Steve Joyce, ambaye ni Daktari wake wa "Internal Medicine". Madaktari wanasema Binti Sadia ni MUUJIZA wa Mungu kutokana na HALI aliyokuwa nayo kabla ya huduma ya UPASUAJI. Asanteni SANA kwa DUA na SALA zenu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages

Contact Form

Name

Email *

Message *