Wednesday, June 28, 2017

CHELSEA YAANZA KUWAUZA VIJANA WAKE KUSAKA FEDHA ZA USAJILI WA BAKAYOKO
Timu ya Chelsea imeanza kuwauza wachezaji wake ili kuwanunua Tiemoue
Bakayoko na Alex Sandro, ambapo sasa wamekuja na mbinu ya kuweka sharti la
kuruhusiwa kuwanunua tena wachezaji vijana inaowauza.
Tayari mchezaji wa Chelsea, Bertrand Traore, amehamia Lyon ya Ufaransa
kwa kitita cha paundi milioni 16 hapo jana, ambapo Chelsea itapata asilimia 15
ya faida iwapo Lyon itaamua kumuuza baadaye.
Timu ya Chelsea pia imeweka kifungu cha kumnunua tena itakapomuhitaji
ili kuepusha kosa walilolifanya kwa Romelu Lukaku, pia beki Nathan Ake
anayewaniwa na Bournemouth kwa kitita cha paundi milioni 20 amewekewa kifungu
hicho.
Bertrand Traore akiwa
ameshatua rasmi katika timu ya Lyon
Chelsea ilimuuza Romelu
Lukaku kwa Everton kwa kitita cha paundi milioni 28 bila kifungu cha kuweza
kununua tena.
Tags
# MICHEZO
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
RayVanny afanya colabo na staa wa muziki Marekani Jason Derulo
Older Article
Chidinma amtaja Ali Kiba kama msanii anayetaka kufanya naye colabo Afrika Mashariki
TAARIFA KUTOKA BODI YA LIGI KUU TANZANIA
Hassani MakeroMar 08, 2025WAKAZI WA DAR WAJITOKEZA KUCHUKUA NAMBA KUSHIRIKI MBIO ZA YAS KILI INTANATION HALF MARATHON
kilole mzeeFeb 15, 2025KOCHA WA YANGA APEWA MKONO WA KWAHERI
Hassani MakeroFeb 04, 2025
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment