Friday, April 27, 2018

Boti Yapinduka Ziwa Victoria na Kuua Wawili
Watu wawili wamefariki dunia baada ya boti waliyokuwa wakitumia kusafiria kupinduka. Ilipokumbwa na dhoruba kali katika ziwa Victoria, Sengerema jijini Mwanza.
Akizungumza kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, amesema boti hiyo ilikuwa na jumla ya watu watano ambao walikuwa wa wakisafiri kutoka Sengerema kuja Mwanza, na ndipo ilipokumbwa na dhoruba wakiwa njiani, na kusababisha boti hiyo kupinduka na watu hao kufariki.
“Kuna boti ilikuwa inatoka Sengerema kuja huku Mwanza, ilikuwa imebeba mkaa pamoja na udaga, walivyokwenda kama robo safari yao hali ya hewa ikawa mbaya kukawa na dhoruba, wakiwa wanageuza wanarudi ikawa shida ikapinduka, ndani ya hiyo boti kulikwa na watu watano, wanaume wanne mwanamke mmoja, watatu waliweza kuogelea lakini hawa wawili walishindwa, mwanamke na mwanaume mmoja, majina bado sijayapata”, amesema Kamanda Msangi.
Kamanda Msangi amesema miili ya watu hao imepatikana, na wanafanya utaratibu wa kuihifadhi hospitali, ili ndugu waweze kuitambua na kuichukua kwenda kuzika.
Tags
# KITAIFA
Share This
About Hassani Makero
Hassani Makero is a Wor'Out Media Country Manager located at Unguja-Zanzibar, Tanzania performing all technical issues concerning of Media Broadcasting activities, Satellites, and FM and Television equipments supplier.
Aside from that, Hassani Makero is also a Writer, Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 10 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs.
Aside from all above he own and operate his Blog known as Wor’Out Media since 2014.
Newer Article
Majonzi Yatawala, Kuagwa Kwa Mwili Wa Mtoto Aliyechomwa Kisu Na Dada Yake
Older Article
COCA-COLA NYANZA BOTTLERS YAMWAGA ZAWADI ZA PROMOSHENI YA 'MZUKA WA SOKA'
Uchambuzi wa bajeti kuchochea ufanisi taasisi za umma
Hassani MakeroMar 24, 2025KAMPENI YA 'NO REFORM NO ELECTION' YAPOTEZA MWELEKEO RUKWA
Hassani MakeroMar 24, 2025TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI KUFANYIKA MIKOA YOTE TANZANIA
Hassani MakeroMar 24, 2025
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment